Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 7,923
- 13,405
Waungwana salamu
Nisipoteze muda mwingi niende moja kwa moja kwenye mada.
Kujiuzuru uspika kwa Mhe. Ndugai kumezidi kuonesha ni kwa namna gani kama Taifa bado hatufahamu mambo mengi ya kisiasa, kiutawala, uraia na kiutendaji.
Wapo waliombeza Mhe. Ndugai wapo walioshitushwa na wapo walioangalia kujiuzuru kwake kama fursa kisiasa na hawa ndio lengo la mada yangu japo wengine nitaongelea kwa uchache sana.
Wanasiasa wetu bado wanasiasa za ama kubahatisha au siasa zisizo na mikakati ya muda mrefu. Bila kupepesa nimuongelee mhe. Tulia.
Binafsi nadhani asingechukua fomu ya kuwania uspika kwa sasa, huu ni moja ya mkakati mbovu aliowahi kupanga.
Ipo wazi Mhe. Tulia ni ngumu kwake kuukwaa uspika na hili si kwamba hawezi kufanya kazi hapana ni kutokana tu na muundo wa awamu ya sasa unampa wakati mgumu sana kuwa spika wa bunge.
Mbaya zaidi uwezekano wa Mhe. Tulia kubaki kuwa mbunge pekee ni mkubwa pia. Nadhani alipaswa kutulia asome mchezo asubiri 2025 kama uhai ukiwepo aingie mchakatoni.
Hili somo liwaguse wanasiasa wote hasa vijana, ikitokea nafasi ya ama uchaguzi au kinyang'anyiro chochote kama haukuwa na mpango nao bora ukaacha ikakupita, siasa sio mchezo wa bahati nasibu ni mipango na mikakati.
Kama ukiona kila nafasi zikitokea unataka kugombea jua bado haujaijua siasa unayoifanya, jipange vizuri.
Kila la kheri