evonik
JF-Expert Member
- Jun 12, 2015
- 3,996
- 5,189
Heshima kwenu wakuu,
Poleni kwa majukumu ya kazi, maisha yaenda hivovo hata iweje kikubwa unaishi na pumzi ipo.
Niingie kwa mada moja kwa moja. Sisi binadamu ni viumbe ambao kwa kweli haturidhiki hata iweje hautuwezi kuridhika na usitegemee hata siku moja kumridhisha mtu utaumia sana.
Ipo hivi, siku moja jamaa mmoja aliniachia ofisi yake nisimamie, kuna watu walikuwa wanafanya kazi kuanzia asubuhi hadi jioni, sasa ikafika wakati wa chakula cha mchana, hao wafanyakazi wakawa hawana hela ya chakula. Niikawaambia niwape elfu kumi yangu, boss akija atanirudishia mimi hela yangu kwa kukatwa kwenye malipo yenu.
Wakawa hawataki wanataka 20 elfu, nikawaambia ngoja nimpigie boss mumwambie wenyewe, nikampigia boss wakamwambia,boss akagoma kuwapa, akaniambia nisiwape pesa yoyote hadi yeye (boss) atakaporudi, basi wakanirudia tena kuitaka ile elfu 10, kiukweli nilikasirika nikawaambia siwapi hata senti kumi,basi wakashinda njaa wakifanya ile kazi hadi mida ya jioni boss aliporud ndio akawatoa hela yao.
Siku nyingine kuna dada mmoja kanipa kazi nimfanyie (free) mtandaoni, basi ikapita kama dakika 10 nikamwambia mtandao unasumbua akanijibu, kwa hiyo nikusaidiaje (alishasau kazi alonipa) ukweli niliumia.
Yapo mengi yaliyofanyika kama hayo, ila nimeona ni bora mtu anione nina roho mbaya tena ya korosha kuliko kuonekana mnafiki na mzandiki (ukizoeana na mtu anakudharau sana). Naamini hivo bora no mzinz sana (tajilinda) kuliko niwe mlevi sana(sorry kwa wanywaji)
(Picha ya mwanaume ni mfano tu)