Mambo 10 kuzingatia ili mpenzi wako aanimi kuwa unampenda kwa Malengo

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Kumpa uhuru wa kuhoji na kukushauri katika maisha yako.
Asiwe kama mlinzi wa getini, kila kitu ni honi na muda wa kujua sasa ni saa 6 natakiwa kwenda kula na chochote akutacho kuta hana haki ya kuhoji ni kula ama aache. Mpenzi mwenye kupewa uhuru wa kuhoji na kushauri huwa na imani ya leo na kesho nawe.

2. Kumshirikisha katika mfumo wako wa utafutaji.
Wanaume wengi hawapendi wanawake zao wajue wanachopata, kwa mtu mwenye malengo naye ni jambo jema akijua unakazi gani, biashara gani, au unakitu gani cha kukuingizia. Nafasi hii uonyesha uko naye kwa malengo ya familia endelevu.

3. Kujali watu wake wa karibu iwe marafiki, ndugu na familia.
Unapomwambia unampenda na unachukia familia yake, huu ni uongo na hata ikiwa ni kijitabia, basi ujue una choyo acha. Kuwapenda watu wa karibu ni kumaanisha, upo tayari kumtetea na kumlinda na maisha yake.

4. Kumtambua hulka zake.
Itakufanya usimshangae mabaya na mazuri yake, usipomtambua huwezi ishi kwa mipaka naye na hata inapotokea amekukosea ni ngumu kujua namna ya kuthibiti hasira yako. Ni rahisi kufanya muauzi na baadae kujilaumu.

5. Kumjali kihisia na kimazingira.
Choyo, ubinafsi, kujitia uoni, huna hamu na kitu au jambo fulani. Pindi unapokuwa na mwenza upaswi kuishi nayo hayo. Ni lazima uishi katika wingi wa sisi, kujali hisia za mwenzio na mahitaji yake ya kimazingira.

6. Kumsamehe na kuyapuuza mengine yasio tija.
Unaishi na binadamu siyo malaika, tegemea pande zote za shilingi, kununa nuna, kukumbushia makosa, kuyatazama yaliyopita na kuwa na moyo mgumu wa kusamehe huku utaki aende, ni kuishi katika penzi lisiloweza kukua.

7. Kuacha kumchunguza
Kumchunga mtu mzima ni kama kuchezea nyeti zako, kama anaamua kutulia atatulia ila akiamua kuuwasha moto basi atauwasha, la msingi mueleze wazi usichopenda na mkemee pale unapoona anakuwa kinyume nawe. Mwenye akili na utayari ataelewa unachomaanisha, mtu mzima kuchungwa ni ishu.

8. Kujiongeza na kuwa romantiki.
Acha kupenda kila kitu kuombwa ombwa, kila jambo ukumbushwe kumbushwe, kila jambo mpaka uwe na shida wewe ndiyo uone tija. Msome uliyenaye na mtambue.

9. Kumheshimisha Kwa marafiki, ndugu na familia yako.
Mbaya kuambiwa unapendwa alafu hata akiondoka hujui utampatia wapi wala hujui utamuuliza nani juu yake. Unaposhindwa kutatua jambo naye hujui pia mtu wa kwenda kumshtakia na mwenye kuweza kumuita. Ni tatizo

10. Kuzitambua ndoto zake.
Maendeleo ni ya wote, kushikana mikono ni tija na jambo kubwa la kujenga mapenzi bora. Hivyo, una malengo basi zingatia hayo, mmngine matokeo muachie Mungu.
textgram_1675868774.jpg
 
Ngoja aje yule jamaa wa,,, NASEMAJEEEE NASEMAJEEEEE MANENO KIDOGO PESA MINGI.
Hahaha kaka Alphonce, yaan kuna watu wanasema pesa ndiyo mapenzi lakini wenyewe wanao wapenzi na unakuta wanachakata papuchi bila pesa na mbaya zaid wale wenye pesa kidunia wote watalaka ni hali tete " aligundua pesa mwenyewe amekufa na madeni" hahaha siyo maneno yangu ni stamina.
 
Hahaha kaka Alphonce, yaan kuna watu wanasema pesa ndiyo mapenzi lakini wenyewe wanao wapenzi na unakuta wanachakata papuchi bila pesa na mbaya zaid wale wenye pesa kidunia wote watalaka ni hali tete " aligundua pesa mwenyewe amekufa na madeni" hahaha siyo maneno yangu ni stamina.
Mwenye pesa anachapiwa na ka-huni kasiko na pesa, kasiko na pesa kanachapiwa na muhuni mwenye pesa,, MAPENZI KONYO SANA.
 
Back
Top Bottom