Bima ya afya (NHIF) kwa hili sio sahihi mnatuibia

Bima ya afya (NHIF) kwa hili sio sahihi mnatuibia

Dogo acha kulalamika sana,

Kwa sheria za NHIF
Dependant ni watoto wako wa kuzaa,

Hizi sheria hufanyiwa mabadiliko kunapokuwa na ulazima,

NHIF wameweka utaratibu mzuri kuwa
Wastáafu,

mzee akistáafu atapewa bima yake special ya kustáafu yeye na mke wake !

Nitajie bima gani ingine inatoa kadi za matibabu kwa watumishi wao walio stáafu kazi
AAR
Jubilee
Strategis
Momentum
Etc
NHIF ni mfuko wa bima wa taifa kwaiyo ulitakiwa uwe na wigo mpana zaidi kufikia wananchi walio wengi.kwaiyo hizo changamoto anazosema mdau nizakufanyia kazi sio kuanza kufananisha na vitu vingine.
 
NHIF ni mfuko wa bima wa taifa kwaiyo ulitakiwa uwe na wigo mpana zaidi kufikia wananchi walio wengi.kwaiyo hizo changamoto anazosema mdau nizakufanyia kazi sio kuanza kufananisha na vitu vingine.
Elimu tunatoa sana,
Huko vijijini wana hizi
CHF

Kazi ni kwako
 
walijuaje ww siyo mtoto wa mwenye bima? mim naitwa JONI KACHELO,ww unaitwa JAJI J.KACHERO(iwe ni kuzaa au siyo lazima tu utatumia jina yangu)
 
kama alishastaafu huwa anabaki na kadi mbili tu ya kwake na mke wake tu ,tena mke iwe inatambulika maana kuna ishu kama za vyeti vya ndoa na sio kimada,utaratibu upo siku nyingi sana
 
mlezi wako anapaswa kurudisha kadi nyingine zote za Watoto kabla hajapigwa reject na yeye ,arudishe apewe nyingine yake na ya mkewe
 
tunawasisitiza sana kwenye bima kuna kitu inaitwa utmost good faith(uberimae fidei) kua wa kwel na kufuta mkataba unasemaje and to disclose all material fact
 
dakika saba tayari nipo ofisi za Bima nikauliza mbona imekuwa hivi hospitali nilikotoka wakaniuliza Bima yangu nani alikata nikamtajia ni mlezi wangu, wakasema utaratibu umebadilika siku hizi anaetakiwa kukukatia ni mzazi pekee, nikamwambia mlezi mwenyewe alikuwa hana mtoto hata mmoja na mimi ndie niliekuwa kama mtoto wake wakanijibu hiyo haijalishi.

Ni majizi, ni kama vile wanatoa hisani kumbe ni haki ya wachangiaji, wananunua magari ya kifahari badala ya fedha hiyo kuboreshea huduma kwa watanzania, mbaya zaidi bima yenyewe ni ya kulazimishwa, wangeacha watu wachague namna ya kutibiwa kwa hiari badala ya wafanyavyo, binafsi naona kama wanabaka.

Kama utaratibu umebadilika wanaona shida gani kutangaza kwenye vyombo vya habari kwa kuorodhesha kadi zisizo qualify kupata huduma ili wategemezi wasiende kuwa rejected hospitali wakiwa wanaumwa na wanamatumaini ya kutibiwa?

nchi za wenzetu zinapigania ustawi wa raia wake, lakini hapa kwetu walioopewa dhamana ya kushughulikia ustawi wa raia wanatazama kujineemesha wao kwanza kupitia makusanyo ya wadau, mbaya zaidi wanakosa ubunifu wa kufanya maboresho, jambo rahisi kulifanya kwao ni kuwatesha raia kwa kuwanyima huduma.

I hate NHIF, ni bora ifumuliwe na kuanzishwa kitu kingine
 
Hawa NHIF si wako chini ya serikali Hawa!.
Hivi ujawai kujiuliza swali hili?" Ni huduma IPI ya kijamii itolewayo na serikali iliyo bora" ..jibu ni hakuna ..
Haya hawa NHIF nami walinifanyia hivyo hivyo mpaka Leo...juzi juzi kuna hospitali nilienda nikamkuta daktari kwa Bahati nzuri nilikuwa namfahamu akaniambia nisilipie atafanya maarifa na ntapata huduma free kupitia iyo iyo NHIF..kifupi kuna mbinu mpya wanawapiga vizuri sana NHIF..nilifurahi sana na jamaa akaniweka wazi kuwa ndio grisi iyo wanayoitumia..hakuna sababu ya kueleza wanapigwaje watashtuka acha wapigwe tu
 
Dogo acha kulalamika sana,

Kwa sheria za NHIF
Dependant ni watoto wako wa kuzaa,

Hizi sheria hufanyiwa mabadiliko kunapokuwa na ulazima,

NHIF wameweka utaratibu mzuri kuwa
Wastáafu,

mzee akistáafu atapewa bima yake special ya kustáafu yeye na mke wake !

Nitajie bima gani ingine inatoa kadi za matibabu kwa watumishi wao walio stáafu kazi
AAR
Jubilee
Strategis
Momentum
Etc
Kiongozi yaelekea wewe una ufahamu katika taratibu za nhif, hebu nijuze kama hali ndiyo kwamba dependant ni watoto wako wa kuzaa vipi kuhusu wale watoto wetu ambao ni mayatima pia kuna wajane ambao wako kwenye utegemezi wetu?
 
Hawa NHIF si wako chini ya serikali Hawa!.
Hivi ujawai kujiuliza swali hili?" Ni huduma IPI ya kijamii itolewayo na serikali iliyo bora" ..jibu ni hakuna ..
Haya hawa NHIF nami walinifanyia hivyo hivyo mpaka Leo...juzi juzi kuna hospitali nilienda nikamkuta daktari kwa Bahati nzuri nilikuwa namfahamu akaniambia nisilipie atafanya maarifa na ntapata huduma free kupitia iyo iyo NHIF..kifupi kuna mbinu mpya wanawapiga vizuri sana NHIF..nilifurahi sana na jamaa akaniweka wazi kuwa ndio grisi iyo wanayoitumia..hakuna sababu ya kueleza wanapigwaje watashtuka acha wapigwe tu
Mkuu usiwafichulie njia yao, vyuma vinakaza sana
 
Usihangaike na ma bima, ukiugua waite shilawadu waki report kipindi we andaa tenga la pesa kutoka ikulu, mwenzako Wastara alipata milioni 37, anaumwa mguu na alipelekwa india.
Acheni kung'ang'ana na mikadi ya bima na kulalamika, jiongeze mkuu anakesha shilawadu hao ndio mpango mzima.
Ukiumwa kichwa, koo linawasha wajulishe SHILAWADU.
Duuh ID yako mkuu. ..!
 
Angalizo!!!!!! Hivi mmekwisha wahi kuona matumizi ya watumishi wa NHIF wakiwa ofisini??? kwa uchache, hawa watu wananunuliwa maji ya kunywa na wanapeleka majumbani kwao, hawa watu matumizi ya anasa ofisini ni usipime, maziwa ya kopo kila mtumishi kupeleka nyumbani, yaani gharama zooote hizo wanatoa katika michngo yetu alafu huduma wanatupa kiduuuchu. Vinatia uchungu hebu chunguzeni wenyewe ktk haya maofisi mtayaona haya
 
Huwa najiuliza haya makampuni huwa hayafanyiwi Auditing. Maana haya makampuni ya serikali huwa yanageuza baadhi ya ofisi Kama mali zao na family zao
 
Kumbe hii habari ya baadhi ya kadi za NHIF kukataliwa ni kweli?! Jana nilimsikia mtu mmoja akilalamika kwamba alienda hospitali akiwa na kadi ya bima ya NHIF aliyokatiwa na mke wake wa ndoa ambaye bado ni mwajiriwa lakini kwenye system ilisomeka "rejected". Sasa hiyo kiutaratibu ni sahihi kweli?
 
walichofanya ni kusitisha bima ambazo hazina wachangiaji. mlezi akishastaafu nani anailipia hiyo bima? ni wazi kwamba itakuwa ilikuwa inatumika buree. kwa maneno mengine ni kwamba wameamua kutoa huduma kwa kadi zinazochangiwa tuu.
Kwani yeye kasema Mlezi wake alikuwa hachangii? Kufanya hivyo kwa watu waliostaafu at least ina-make sense lakini siyo kwa mlezi ambaye yupo na anachangia halafu mtegemezi asitibiwe eti tu kwa sababu huyo mchangiaji siyo mzazi wake. Wanatuibia sana hawa NHIF
 
Umeeleza mambo 2 lipi hasa lililosababisha bima yako ikataliwe.

-wazee kustaafu au
- wewe kuwa Tegemezi.
 
LUFUNGULO K upo zaidi kutetea, najua wewe ni mtumishi wa NHIF lakini pokea maoni ya wadau uyafanyie kazi sio kuendekeza ubishi.
 
Back
Top Bottom