bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,016
- 4,961
Mfuko wa afya wa bima ya afya wameleta mabadiliko ambayo wengi hatukutarajia, sijajua shida ni uchumi kuwa mbaya au sababu ni nini haswa.
leo nimetoka hospitali kutibiwa nikatoa kadi yangu mapokezi kama kawaida wakati nasubiri kuitwa kama ilivyo ada,nikaitwa nikaambiwa kadi yako ya bima imekataliwa nikauliza sababu sikupewa nikatoka hapo chapu nikaenda hospitali nyingine kubwa tu wanayotumia bima, basi nikatoa kadi kama kawaida wakati nasubiri kuitwa muda ukafika nikaitwa nikaambiwa kuwa kadi yangu ya bima imekuwa rejected nikauliza kivip nikaambiwa niende hapo zilipo ofisi za bima vile sio mbali nikaulize sababu.
dakika saba tayari nipo ofisi za Bima nikauliza mbona imekuwa hivi hospitali nilikotoka wakaniuliza Bima yangu nani alikata nikamtajia ni mlezi wangu, wakasema utaratibu umebadilika siku hizi anaetakiwa kukukatia ni mzazi pekee, nikamwambia mlezi mwenyewe alikuwa hana mtoto hata mmoja na mimi ndie niliekuwa kama mtoto wake wakanijibu hiyo haijalishi.
la pili wanadai pale mtu anapostaafu basi wale wategemezi wake hawana chao tena ,yani ukomo wa matumizi ya bima ndo unafikia hapo.
sasa nauliza huu utaratibu wa aina hii unalenga kumnufaisha nani?
yani kila sehemu pamebanwa hamna hata pa kukimbilia kwa sasa.
alichosema mzee watu wataishi kama masheatani nimeamini.
=====
UPDATE:
=====
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), unapenda kufafanua juu ya taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa baadhi ya taratibu za Mfuko katika utoaji wa huduma zinalenga kuwaibia wanachama. Madai hayo sio ya kweli na Mfuko unapenda kufafanua Taratibu sahihi zilizopo kwa lengo la kufanikisha utoaji wa huduma kwa wanachama wake kama ifuatavyo;
Habari zaidi soma=>Ufafanuzi juu ya suala la wategemezi wa wanachama wa NHIF, wanachama wastaafu