Bima ya afya kwa nini wanafanya hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bima ya afya kwa nini wanafanya hivi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FadStar, Dec 26, 2011.

 1. F

  FadStar Member

  #1
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Bima ya Afya wananikera sana yaani toka nimeomba kupewa kadi sasa ni mwezi wa saba hawajanitengenezea wakati kwenye mshahara hela yao wananikata. Mbona huu ni wizi wa mchana kweupe au maombi ya huku mikoani hajashughulikiwi?
   
 2. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,454
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hicho kitambulisho wala haitaji kutoa rushwa. Ukichelewa sana ni mwezi mmoja tu.
   
 3. F

  FadStar Member

  #3
  Dec 26, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa hawako siriasi kabisa koz tuko mwengi wenye tatizo hilo lakin hawataki kutushughulikia huku pesa yao wakikata kama kawa.
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huenda maombi yenu hayakufika Makao Makuu. Mbaneni mwakilishi wa Kanda yenu ajiridhishe iwapo maombi yenu yalipelekwa na kupokelewa Makao Makuu ya NHIF.
   
 5. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  wewe cha mtoto, mimi niliomba kitambulisho nikiwa na employer mmoja ikachukua kama miezi3, wala sikupata, sasa nipo na employer mwingine na ni zaidi ya miezi4, cjapata hata mara moja na ninaomba na kupeleka form mwenyewe. Hawa jamaa cjui wanafanyaje kazi??? Mi nafikiri serikali ingeondoa monopoly wa NHIF, wanakera na kuboa!
   
 6. n

  nyangau Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huenda mwajiri wako hajazifikisha fomu zako ofisi za NHIF. Lakini zikishafika pale hata hazichukui muda unapata. Nami nilipata tatizo hilo nilipoenda ofisini kwao wakasema fomu zangu hazijafika ikabidi nitoke na mtu wa NHIF mpaka ofisini kwangu na kweli nikazikuta kule
   
 7. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakubaliana nawe kabisa, wanaochelewesha mchakato mzima waajiri na si NHIF.Tatizo kwenye hizi ofisi zetu hasa za serikali kuna urasimu kubwa hata kwenye mambo madogo madogo.Just imagine mtu anaajiriwa leo lkn mshahara ni mpaka baada ya miezi sita kama si uzembe ni nini? ukija kuchunguza utagundua kuwa document zinachelewa kufika hazina.

  Hata hivyo NHIF wameweka utaratibu wa kupata tiba hata kama bado hujapata kadi hivyo nenda kwenye ofisi zao.
   
Loading...