hata mimi
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 1,356
- 1,448
Yaani mtu unajieleza weee halafu daktari anakwambia nenda maabara ukifika eti unapimwa malaria.
Daktari ukimwambia akupime na vitu fulani fulani anakataa tena mwingine anaona kama unamfundisha kazi. Yaani mtu kuandika tu ukapimwe kitu fulani anaona kama anafanya kazi ya mkwe!
Dawa kila siku ni amoxicillin piriton alu na paracetamol ndizo zilizopo. Dawa nyingi unaambiwa ukanunue
Halafu kuna kero nyingine nayo ngoja niiweke humu...
Zamani ukienda hospital fasta tu ila saivi utasotea hapo nje ukisubiri eti wamalize usafi
Usafi ukiisha wanaanza kupanga ofisi zao unakuta karibu lisaa eti wanaandaa. Mapokezi hapo foleni yake ya kufa raia na pale huwa hawana hiyana akianza kaanza
Ukitoka mapokezi unaambiwa nenda kwa daktari huko kwa daktari ndo utalia sasa. Kwanza chumba chenye uhakika wa kuwepo daktari unakuta ni kimoja tu wakati kuna milango karibu saba na yote imeandikwa chumba cha daktari.
Basi mnafika mnajazana hapo kwenye chumba cha daktari na si ajabu hayupo mpaka anakuja kuwasikiliza ni lisaa lingine mbele. Mkitoka ngwe hiyo mnakwenda kupigishwa mark time maabara nako tena
Maabara ndo kabisa kama una moyo wa hasira hutadumu yaani. Kwanza mpaka ashike hizo document zenu ni kipengele na Jamaa kisha anachukua makaratasi yenu yote anaita mmoja mmoja anawatoboa vidole na kuwapa vichupa (malaria na mkojo ndo vipimo maarufu utakavyopimwa ukifika maabara)
Ngoma majibu sasa badala atoe kwa kadiri anavyowapima eti anasubiri karibu awamalize wote ndipo utasikia akiwapa majibu mrudishe kwa daktari
Maana yake mwendapanga foleni upya kwa daktari tena. Mkitoka hapo mnaenda kupigishwa foleni kwenye dawa napo
Siku moja nimeenda Ruangwa Hospital aisee asubuhi sana nikakaa pale nje usafi wakaja kumaliza saa saa 2:30 okay tumejipanga kwenye mabenchi wakaanza kuweka vitu hapo kama haikuchukua saa na nusu sijui tukavumilia
Wameanza huduma tena wagonjwa kwenda kwenye milango ya madaktari hakuna dokta hata mmoja nakumbuka alikuja daktari mmoja kwenye kama saa nne hivi ndo akaanza kuhudumia.
Kwenda maabara nakumbuka tukamkuta mdada wa usafi anafanya usafi tulikaa pale nje kama wehu mara jamaa anavuka mara anarudi baadae ndo akaja kuchukua makaratasi hayo akapima watu weee wakaisha waliokwepo pale
Basi tulikaa pale aisee mpaka unawaonea huruma wale wagonjwa waliozidiwa. Jamaa kaja kuwapa majibu sijui saa saba halafu ndo foleni kwa daktari tena halafu foleni zinakuwa mbili sasa ya wapya wanaoingià kwa daktari na wanaorudisha majibu yaani balaa tupu
Tuache yote hayo narudi kwenye topic yangu ni kwamba TUKIONDOA VIHOMA VIDOGOVIDOGO HIVI VYA KAWAIDA NA KULAZWA- BILI YA KITANDA, UKIONDOA HIVYO VITU VIWILI BIMA YA AFYA HOSPITALINI (ZAHANATI, KITUO CHA AFYA NA HOSPITAL) HAINA MSAADA WOWOTE NI UJINGA TU