Bima ya Afya ni wezi kama wezi wengine, sijaona sababu ya wao kuweka masharti kwenye fedha ya mtu mwingine, wanatumia fedha zetu kufanya vikao na kujilipa posho kwenye mahotel makubwa, huku sisi wachangiaji tunapata huduma hafifu kwenye hospitali tunazoambiwa tukapate huduma, wananunua mashangingi ya bei mbaya wakati sisi tunakosa dawa hospitalini na hata baadhi ya waganga kututaka kutoa rushwa kwa kisingizio cha bima ya afya hailipii huduma hiyo, ukipiga simu kufuatilia haki yako unajibiwa siasa,
Binafsi sioni umuhimu wa kuwa na hawa bima ya afya maana wamekaa kiudalali zaidi kuliko huduma kwa raia, binafsi ningependekeza uanzishwe mfumo wa fedha zetu za michango kwenda kwenye account maalum ambayo itakuwa na smart card itakayo muwezesha client kuwasilisha card husika kwenye hospitali husika na malipo kutolewa moja kwa moja toka kwenye account na salio kubakia humo badala ya malipo kufanywa na wakala ambaye matumizi yake ni makubwa kuliko mchangiaji