Aina za Bima ziko nyingi, Ila kwa swala lako niseme ziko mbili tu, Bima ndogo na Bima kubwa. Kizungu ndio hiyo"Third party" na "Comprehensive".
Third party/Bima Ndogo faida yake ni kua bei/gharama yake ni rahisi tu. Hasara yake ni kwamba ikitokea jambo lolote baya (kuibiwa/ajali/kuungua) kuhusu chombo chako, yenyewe itamfidia "Kitu/Mtu" wa tatu tu. Wewe dereva na Chombo chako hamtahusika katika kufidiwa huko.
Comprehensive/Bima kubwa hii ni kua ikitokea jambo lolote baya (kuibiwa/ajali/kuungua) kuhusu chombo chako yenyewe itamfidia kila alieathirika na ajali hiyo ukiwemo wewe dereva pia. Na chombo chako kama kimepata madhara nacho kitafidiwa pia.
"Kitu/Mtu" wa tatu ni Nani? Hapa wewe unaendesha hicho chombo/Bajaji Ni wa Kwanza. Chombo/Bajaji yako ni ya pili, utakae msababishia ajali iwe ni mtembea kwa miguu, au chombo cha moto au hata nyumba, kibanda umegonga ndio "Kitu/Mtu" wa tatu.