Billionea Davis Mosha

Huyu jamaaa nawanyonya sana wafanyakaz wake hasa madereva, mshahara anawalipa tr 17-23 sasa nn fahar yake?
 
Habari Za Muda Wana Jf Nina Habari Nimezisikia Chini Ya Kapeni Kuwa Bwana Mkubwa C.E.O Wa Dellina Mr Davis Mosha Amenunua Gari Aina Bugati? Je Ni Za Kweli Maana Huyu Bwana Mkubwa Kwa Magari Ya Nadhani Anaongoza

Fanya yako. Unajua hela anapata kwa mazingira gan ?? Mjini hapa dogo.....
 
Mkuu Filipo,
Acha nikuunge mkono tu ndugu yangu. Ungejua kuwa aendapo nyumbani anapita barabara isiyopitika ungejinyamazia tu. Miye huwa nawashangaa hawa wachaga wenye vitambi wakati kwao hakuendeki, kweli ana kajumba kake kazuri lakini jumba bila njia ya kwenda huko ni faida gani? Hapo mbele ya uso wa nyumba tu kuna kashule kake alikosomea Elim ya msingi, watoto wanachezea mpira kwenye mteremko wa ajabu. Kama umeshindwa hata kulipia greda liwatengenezee watoto wako uanja tena walio nao, kama umeshindwa kuweka kalami barabara yako unayo itumia kwenda nyumbani kama nusu km huku unajiita bilionea, sijui ubilionea ni wa tarakimu au nini.
Hongera zake lakini atumie baadhi ya hizo njuluku atengeneze sifa kwao wamjue si darisalama kule Yanga
 
sasa habari usisikie wewe uje kutuuliza sisi
 
Wapo ndugu zake kibao hawana pesa ni masikini wakubwa ni bora angewanyenyua kwanza kabla ya kununua magari hayo.
 
Kule YANGA sports club alikimbia Mizinga ya Wanachama, devis ni m-bahili sana hapendi kuwasaidia wengine wala ndugu.
 
Huyu jamaaa nawanyonya sana wafanyakaz wake hasa madereva, mshahara anawalipa tr 17-23 sasa nn fahar yake?

Fahari yake ni Magari pasipo masilahi ya wafanyakazi wake, yeye hawajali bali anajali ufahari wake binafsi.
 
Jamani, katika maisha kila mtu anakipaumbele chake, sio kusaidia ndg, mara barabara yakwenda kwao, mara shule, sio kwamba havioni ila sio kipaumbele chake. Maisha jayana fomula moja.
 
Kwa hiyo kama watu wengine ni masikini ndo mtu asifanye yake? Mbona fikra za kimaskini hizi jamaangu
 
Kule YANGA sports club alikimbia Mizinga ya Wanachama, devis ni m-bahili sana hapendi kuwasaidia wengine wala ndugu.

Yani mtu asifanye kazi ategemee ndugu yake ansaidie?
 
Habari Za Muda Wana Jf Nina Habari Nimezisikia Chini Ya Kapeni Kuwa Bwana Mkubwa C.E.O Wa Dellina Mr Davis Mosha Amenunua Gari Aina Bugati? Je Ni Za Kweli Maana Huyu Bwana Mkubwa Kwa Magari Ya Nadhani Anaongoza

Kijana fanya kazi uisaidie familia yako kutoka kwenye lindi la umaskini, ushabiki wa kitoto huo, akinunua au asinunue wewe inakuongezea nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…