Billboard Afrobeat chart top 50

Afrobeat ni mziki wa West Africa. Ningeshangaa kuona watu wasio wawest africa kuwa kwenye hiyo list.

Siku kukiwa na chart ya bongo fleva nitashangaa kuona wawest africa humo.

Endeleeni kuimba amapiano au kama wanaija mkidhani mnaenda global kumbe mnaonekana kituko tu. Huwezi kushindana na mtu kwenye uwanja wake wa nyumbani ukamshinda it's that simple.
Tatizo pia mziki wetu hauna Utambulisho tunaimba midundo yyte ilimradi unatrend sehemu zingine.
 
Tatizo pia mziki wetu hauna Utambulisho tunaimba midundo yyte ilimradi unatrend sehemu zingine.

Bongo fleva ina utambulisho wake timamu kabisa. Swala ni watu kuiga genre zingine na kutaka kuwa kwenye hizo charts badala ya kutop genres zenu that will never happen. Mnaija hawezi mshinda mbongo kuimba bongo fleva.
 
Kuna wasanii wengi wakubwa toka Ghana, South Africa na Kenya hawapo kwenye hiyo list. Ni suala la upendeleo wamefanya nahisi sababu ni wanaijeria wanaoandaa hiyo list.

Afrobeats ni mziki wa West Africa mainly Nigeria.
Bongo fleva - TZ.
Genge - KE.
Amapiano - SA.
Bolingo - Congo.
Nk nk.

Inawezekana mziki wetu bado haujakua hivyo ila kusema haujakua sababu hatupo kwenye charts za Afrobeats is comparing oranges to apples.

Ningeshangaa zaidi kukuta mtu asiye muwest Africa kwenye hiyo list kama ambavyo nitashangaa kuona mnaija kwenye list ya bongo fleva. Huwezi mshinda mtu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
 
Sijashangaa, nimeuliza..
Umeshangaa, jinsi ivyouliza inaonyesha umeshangaa lakini all in all swali la kujiuliza je nchi zote za Africa hazijui muziki? Africa ina nchi 54 na kwa nini Wapopo ndiyo wazitawale chats? Issue si Tanzania peke yake bali nchi zote zilizokosekana kwenye hiyo chart.
 
Waanzilishi wa hiyo idea Ni wanaijeria. Think about it again.
Mpaka ameifuatilia hiyo orodha ina maana hilo analijua, Wapopo wanaoishi Marekani ndiyo wanaoandaa hiyo chart.
In short wameangalia zaidi nyimbo zinazopigwa kwenye clubs zao za huko, house-parties zao, na viji-online radios and TVs.
Ili utoboe hapo ni mpaka upenye kwenye soko lao wanaloli-control wao wenyewe.
 
Hao wapangaji wa hiyo chat huko wengi wanigeria unategemea nini haha,,,wenzenu wamejaa huko na UK wacha wawainue ndugu zao,wabongo walioko nje full kubania wenzao anyway hongera zao wanajua na wana stahili!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom