Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu maskini zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga kuku.
Bilionea huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Chanzo: BBC