Bilioni 8 zatengewa viongozi wastaafu akiwemo Lowassa, wakati hospitalli zatengewa bilioni 5 tu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kwa taarifa nilizozipata kupitia chanel 10 muda mfupi uliopita ktk kipindi kilichokuwa na mada inayosema tathimini ya mjadala wa bajeti 2012, Viongozi wastaafu serikalini ambao bila shaka ni maraisi wastaafu na mawaziri wakuu wastaafu wametengewa sh bilioni 8 wakati hospitali kubwa za serikali zimetengewa sh bilioni 5 tu.

Katika jambo lililonishangaza zaidi ni pale mshiriki wa kipindi aliposema kuwa miongoni mwa viongozi hao wastaafu ni pamoja na Edward lowassa.

Sasa swali hapa ni je Edward Lowassa alijiuzulu au alistaafu?Au utaratibu ukoje kwa anayejua?

Kituko kingine cha kuumiza ni nani muhimu wanasiasa wastaafu au ni huduma za afya kwa umma wa watanzania?

Hivi ile hoja ya mh.Mnyika kuhusu udhaifu na kwa mambo kama haya kwanini watu wasiamini kuwa kuna udhaifu?

Hivi hii ni serikali gani isiokuwa na uwezo wa kupanga vipaumbele?

Kwa mambo kama haya unatarajia migomo itaisha nchii hii wakati watu wanaona,wanasikia na kusoma yanayotendeka serikalini?

Hivi watu wakigoma ni kweli wanashawishiwa na vyama vya upinzani au wanashawishiwa na mipango mibovu ya serikali?

Chama legelege huzaa serikali legelege na bunge legelege.
 
Swali la kujiuliza bajeti ya watu MILIONI 40 dhidi ya VIONGOZI wastaafu 8, eh Mungu legeza mioyo ya wote maono yaelekezwe KWA watanzania walio wengi AMEEEEEEEEEN
 
Wa Tz tunacheka na nyani acha tuvune mabua. Viongozi wa nchi hii ni zaidi ya nchi ya kusadikika.
 
Bora tugome wafanyakazi wote, Strike Strike forever maana tunalea USE*******
Nchi hi kumbe ni ya viongozi pekee, kwa nini hawataki kutibiwa Bongo?
 
Sitaki kuamini!!!


images(5).jpg images(5).jpg
 
Hii ndio mimi husema Waafrika Ndivyo Tulivyo - haingii akilini kama tunavyosema ati - Kuvuja kwa Pakacha nafuu ya Mchukuzi!!... methali kama hizi ni za Kitumwa, sii za watu wenye kujali nguvu ya uzalishaji na wajenzi wa nchi zao. Hili linchi letu laana tupu imetupata na sijui kama kuna mganga..
 
Tatizo la Watanzania ni Maneno mengi sana halafu Vitendo sifuri, Hapa yakipangwa hata Mandamano watu wanabakia kukaa Barabarani kutazama mandamano, Na viongozi wanatumia sana huu udhaifu wa Watanzania kuwa waoga kufanya watakalo, na mwisho wa siku mnakuja kuhubiriwa amani,

Haya matatizo yataendelea mpaka pale tutakapo acha kufanyia maandamano kwenye vijiwe vya kahawa na humu ndani, na tusiwaachie wachache kama CDM kufanya kazi pekee yao,
 
Hivi tufanyeje ili wote tutoke barabarani jamani, manake hii imezidi sasa!
 
Siasa za nchi hii zinawanufaisha wanasiasa wa chama tawala. Pesa zote zinaishia kulipana wao. Hakuna mikakati ya maendeleo wala huduma za jamii.
 
Kutaja tu kiasi hakusaidii kushughulika na tatizo. Kwa mfano hizo fedha zilizotengwa zinahusisha nini na nini. Maana najua pia kuna kubadilishiwa gari wakati fulani, gharama za matibabu, gharama za uendeshaji Ofisi zao binafsi, mambo ya ulinzi na mambo mengine kadhaa. Ikinyumbulishwa ndiyo itakuwa rahisi kusema kipi kiondolewe kwenye mafao yao!!

Pia tukumbuke kwamba wastaafu hao hulipwa asilimia themanini ya mshahara ya kiongozi kama yeye aliyeko Madarakani. Kikwete,Mkapa na Mwinyi wanalipwa asilimia themanini ya mshahara wa sasa wa Magufuli.
 
Duh huwa naona bora tuwalipe hata 500b watupishe kuliko kuwalipa mshahara mpka ukomo wa maisha
 
Back
Top Bottom