Bilioni 25.06 kila mwezi mishahara hewa, hii sio nchi masikini.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,611
Wakati akiwa kwenye kampeni rais Magufuli alisema kwamba anajua ni kwanini fedha nyingi zilizopo serikali hazishuki mpaka kuwafikia wananchi.

Ilikuwa ni baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa ndipo alipoongelea suala la mishahara hewa, na akawapa maagizo ya kuhakikisha linafanyika nchi nzima zoezi la kubaini mishahara yote hewa. Ni zoezi ambalo bado linaendelea kutekelezwa.

Juzi bungeni serikali imetoa mrejesho wa zoezi hilo na kusema kwamba kuna wafanyakazi hewa zaidi ya 12,000 ambao wanaingiza mifukoni mwa wafanyakazi wasio wema shilingi za kitanzania bilioni 25.06 kila mwezi.

Hii nchi sio masikini, ni sisi wenyewe ambao tunajiweka kwenye vigezo vyote vya umasikini. Kwa mwezi zinapotea bilioni 25.06, kwa mwaka ni zaidi ya bilioni 300, fedha zinazokwenda kuneemesha watanzania wachache ambao kwa akili zao wanaowaona wote wanaowaibia kama vile ni mbumbumbu mzungu wa reli.

Na hapa tunaongelea mishahara hewa peke yake, bado kuna upigaji mwingi sana ambao kwa mwaka unaweza ukawa unaingiza mabilioni ya fedha kwenye akaunti za wachache na kuwaacha wananchi wengi kwenye lindi zito la umasikini.

Kupambana na mazoea mabaya ni kazi nzito sana, kwani hata wale wanaoonekana kuwa wasafi kwa nje, ndani ya mioyo yao wamejaa dhuluma za kila aina.

Tujaribu kujiuliza wale wazee wasiojiweza pamoja na walemavu wa ngozi ambao hutembelewa na wafanyakazi wa makampuni na mabenki makubwa kwa ajili ya kulishwa chakula cha jioni moja na kupewa zawadi za sabuni, kanga na nguo nyingine, wamedhulumiwa kwa miaka mingapi?.

Tunaweza kujitegemea na tuna kila haki ya kuwa na bajeti ya mwaka ambayo asilimia kubwa ya fedha itatokana na vyanzo vya ndani. Serikali iendelee kupambana na hawa wanaotaka kuishi maisha kama yale wanayoyaona kwenye runinga kwa gharama ya uwepo wa umasikini na hali ya watu kukata tamaa.

Vita dhidi ya ufisadi inazo baraka za kila mtu ambaye kwa njia moja au nyingine ni mhanga wa mfumo huo dhalimu. Ni vita ambayo mpenda nchi lazima ataiombea kwa Mungu iweze kufanikiwa.
 
Umeongea vizuri sana
Hii ni thread bora kabisa kwa mwaka huu kwa upande wangu
Asante
Nimefurah kuona mwisho unamtaka kila mtanzania kuunga mkono vita hii ya rushwa na ubadhirifu.. Hima wote na tupinge unyonyaji bila kujali tofauti ya itikadi za kisiasa..
 
Back
Top Bottom