Bilionea Mo Ibrahim ataka Afrika iache kuombaomba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilionea Mo Ibrahim ataka Afrika iache kuombaomba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 11, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,581
  Trophy Points: 280
  Date::3/11/2009
  Bilionea Mo Ibrahim ataka Afrika iache kuombaomba

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi

  MFANYABIASHARA maarufu duniani Mo Ibrahim, amesema Afrika inapaswa kuongeza nguvu katika kuvutia wawekezaji badala ya kuomba misaada.

  Kauli ya Mo ambaye ni mwanzilishi wa shindano la Tuzo ya Rais Bora barani Afrika, imekuja wakati sehemu kubwa ya nchi za Afrika zikiwa zinategemea misaada ya wafadhili.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mo alisema pamoja na nchi za Afrika kuhitaji msaada lakini bado zenyewe zinahitaji kuongeza nguvu na mikakati ya kujitegemea.

  Kwa mujibu wa Mo, nguvu kubwa zinazotumiwa na Afrika katika kutafuta misaada nje, kama zingetumika kuvutia wawekezaji, ni dhahiri zingewezesha mafanikio makubwa.

  "Afrika inapaswa kuongeza nguvu kwa ajili ya kujitegemea, inatumia nguvu nyingi kuomba misaada," alisema Mo na kuongeza:


  "Ingeweza kupiga hatua kama ingetumia nguvu hizo katika kuvutia wawekezaji barani Afrika."

  Akionyesha msisisitizo, alisema rasilimali nyingi za barani Afrika zinatosha kuliwezesha bara hilo kujijengea misingi ya kujitegemea.

  Kwa mujibu wa Mo, Afrika inaweza kuomba misaada, lakini si kutegemea kwa sehemu kubwa.


  Wakati huo huo, mkutano kati ya nchi za Afrika na IMF umemalizika jana kwa kutoa maazimio mbalimbali, ambayo ni pamoja na kuhakikisha nchi za Afrika zinaendelea kudumisha uhusiano na shirika hilo la fedha na nchi za Afrika kuendelea kutekeleza sera za IMF,

  Azimio lingine ni nchi za Afrika na IMF kuangalia jinsi ya kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kupata uwakilishi wa viongozi wa shirika hilo.

  Mkutano huop ambao uliwashirikisha mawaziri na magavana wa benki kuu barani afrika pamoja na wahisani na IMF ulianza juzi wakizungumzia jinsi ya bara hili linavyoweza kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani.

  Kabla ya kuanza kwa mkuano huo, Mkuruegenzi Mkuu wa IMF, Dominique Struss-Kahn aliitaka tanzania kubuni njia za kujitegema kwa kutumia rasilimali zake na fursa zote za uwekezaji kwa kutengeneza mazingira mazuri yanayoweza kuwavutia

  Wawekezaji badala ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani.

  Wakati huo huo IMF ilisema itafungua ofisi yake nchini kama sehemu ya mpango wake wa kusogeza huduma zake katika nchi za Afrika.

  Mpango huo uliotangazwa juzi ni changamoto muhimu kwa nchi yetu ambayo ilitanganzwa na IMF kuwa moja kati ya nchi zinazotekeleza vizuri sera za uchumi za shirika hilo.

  Kahn alisema Tanzania imefanya vizuri katika kutekeleza sera za uchumi za IMF pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.

  Alifahamisha kuwa Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi (Mkukuta) ni mfano hai wa jinsi Tanzania ianavyofanya vizuri katika kukabiliana na umasiki nchini.

  Kahn alifahamisha kuwa mpango huo pia unatarajiwa kutekelezwa katika nchi kadhaa za ukanda wa Afrika Magharibi.
   
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wetu Ramadhani, katupa mvutano wa mawazo, sijui kamani ni kwa nia ama imetokea tu. Ametupa rai ya MO tujitegemee kwa kuanza kuacha kuomba-omba halafu hapo hapo IMF wanasema MKUKUTA ni mpango mzuri! kazi kweli kweli.

  Tukija kwenye swala zima la kuomba misaada, MO inaibua jambo la muhimu, muda na nguvu tunazopoteza katika kuomba. Kwani misaada haiji tu - lazima tushwawishi, tuandike, na tutafiti ili tuwashawishi watoaji pesa zao zitafikia malengo yao na yetu! Hivi kuna mtu anataarifa za kujua ni nguvu kazi kiasi gani tunapoteza katika kuomba misaada? inawezekana kabisa ingekuwa bora mtu achukue jembe akalime, maana angekuwa ameshavuna mahindi, kachuma na kula ugali.
   
 3. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
 4. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  i used to respect mo ibrahim sana mpaka pale nilijua kuwa utajiri wake ni kwa kushirikiana na mafisadi serikali bongo na nchi nyingi afrika kwenye kuua incumbents ameifanyia fitna TTCL na kuunda celtel tanzania...hovyo tuu huyu..hana jipya!
   
 5. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2009
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kwa mujibu wa Mo, nguvu kubwa zinazotumiwa na Afrika katika kutafuta misaada nje, kama zingetumika kuvutia wawekezaji, ni dhahiri zingewezesha mafanikio makubwa.

  "Afrika inapaswa kuongeza nguvu kwa ajili ya kujitegemea, inatumia nguvu nyingi kuomba misaada," alisema Mo na kuongeza:

  "Ingeweza kupiga hatua kama ingetumia nguvu hizo katika kuvutia wawekezaji barani Afrika."

  Kikwete Kaenda mara dufu Marekani kuomba Misaada, Kaenda EU mara dufu kuomba misaada, Kaenda Asia mara dufu kuomba misaada. Wasomi wengi Tanzania wanatumia muda wao mwingi kuandika paper kuomba misaada,NGO N.K, wananchi wengi wanatumia muda mwingi kuomba change kwa ndugu, jamaa, marafiki, jirani n.k, kazi ipo.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa Bw.Kapinga lakini tukimuangalia Dr.Mo kwa jicho la tatu ni Mwafrika mwenye uchungu na bara lake ameleta mageuzi makubwa sana ya teknolojia ya mawasiliano barani Africa,wengine ni mafisadi na wamepeleka fedha nje ya bara letu kwa manufaa ya wao na familia zao lakini Dr.Mo ana kila sababu ya kuwa mfano wa ....(Yale uliyoyataja katika post yako!) Lakini sasa mapinduzi ya teknolojia barani Afrika ni kielelezo tosha kuwa ni MWAFRIKA WA NGUVU! I remain...
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu mimi nachukia kama nchi na watu wake wanatumia mda wao mwingi ktk kupitisha bakuli!!!!

  Yaani mtu mzima na nguvu zako na heshima yako na hauumwi..basi unakaa barabarani eti nisaidiwe!
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mo kaongea ukweli mtupu, hili ndilo tatizo kubwa la Afrika na nchi kama Tanzania kwa sasa. Lazima tuweke nguvu zote kwenye uwekezaji na kutengeneza kazi mpya kwa ajili ya wananchi wetu.

  Misaada inaweza ikatumika tu kwenye kuongezea hiyo nguvu, kwa mfano misaada ya kusaidia kujenga barabara, bandari nk.

  Hakuna kitu kinachosikitisha kama kuanza kuomba misaada kwa ajili nya kuendeleza ulaji wa kama kuna magari ya fahari nk.

  Watanzania walio wengi kwasasa wanafanya kazi chini ya masaa 15 kwa siku, hii ni kutokana na ukosefu wa kazi, ujinga na uvivu. Tukifanikiwa kuongeza kiwango cha ufanyaji kazi kufikia angalau wastani wa masaa 30 kwa wiki, naamini nchi kama Tanzania itasogea mbele.
   
 9. L

  Lusajo Kyejo Member

  #9
  Mar 12, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bilionea Mo Ibrahim mimi binafsi namkubali na nichangamoto kwa nchi zetu kufanya bidii zaidi ili tuweze kujikwamua na tuna kila sababu ya kufanya mabadiliko maana kama ni madin tunayo,misituntunayo na tunawezaz kuongeza zaidi na zaidi hata tukaweza kusafirisha hayo magogo nje,mbuga za wanyama tunazo na vivutio kadha wa kadha ni wakati wa kujipanga sasa.
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mo Ibrahim amepiga pale pale panapotakiwa. Nchi changa na hasa yetu imekuwa ikitumia rasilimali nyingi kuzunguka duniani kuomba-omba. Nguvu na rasilimali hizo mara nyingi zimekuwa kubwa kuliko kipato halisi kinachopatikana.

  Nadhani maneno haya ya Mo Ibrahim na Struss-Kahn ni kielelezo tosha kuwa juhudi tunazofanya (hasa sisi Watanzania) katika kuomba-omba, ni aibu, hazina manufaa ya kudumu, ni upotevu mkubwa wa juhudi na rasilimali zetu na zaidi ya yote sio jitihada za kujivunia. Ni kashfa kwetu sote tunaoamini katika kutembeza bakuli kwa taasisi na mataifa ya nje.

  Kwa mtazamo wangu, kama Taifa tukiweza kufanya juhudi za pamoja katika kutafuta maendeleo yetu wenyewe (kwa kila mtu kuchangia kwa vitendo), nchi hii ina uwezo wa kuzalisha na kutosheleza mahitaji yake mengi na muhimu ya kiuchumi na kijamii. Endapo serikali na taasisi za ndani zikiaminiana, zikishirikiana na kutumia nguvu kazi na rasilimali zilizopo nchini bila kuwa na tamaa ya mmoja kujilimbikizia mali (Ufisadi), nina uhakika nchi hii ina uwezo mkubwa wa kupiga hatua kuliko nchi nyingi zilizoendelea. Naamini nia ya kisiasa na ushirikishwaji wa jamii haupo kabisa. Kutokuwepo kwa nia hiyo na ushirikishwaji huo ndio sababu kubwa ya kushindwa kufikia malengo yetu yote, hata kama tutaongezewa misaada/mikopo na wahisani kwa aslimia 200%.

  Kama nchi, ni lazima ufike wakati kila mmoja wetu ajiulize ana fanya nini kuchangia maendeleo ya nchi yake. Serikali iweke hali na haki sawa ya uwezekano wa kila mTanzania kushiriki katika jitihada za maendeleo bila kukata tamaa. Hiyo ndio njia ya kweli ya maendeleo ya Afrika.
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri alikuwa anamsema Rais wetu. Maana nguvu anazotumia JK kutafuta misaada angezipeleka kwenye kutafuta wawekezaji naona tungekuwa mbali. Serikali yetu imegeuzwa ombaomba!!!!! Tumesahau ujamaa na kujitegemea!!!!
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Anamaanisha Viongozi wanaliongezea Taifa hasara kwa kusafirisafiri kusaka na kuwinda misada.
   
 13. B

  Bunsen Burner Member

  #13
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  I support MO 100% for his contribution and hard facts to swallow( especially 4we Tanzanians). We spend a lot of time begging instead of put our house in order, work and utilise properly our resources for the benefit of our entire nation! the countries like Botswana, Namibia where i had an opportunity to work, they are very serious on governance and development, as well as protecting and trying to utilise the few resources they have in order to uplift the standard of life of its people and they always say they dont need grants and loans as basic necessity for their development. We are always go for unnecessary expenditures like BOT towers as if we are a rich nation.I can tell u if see Botswana central Bank building, u will never believe, because it is just a simple three storey building of blocks but ours......( showing off), while we starving!!!.Our priorities are always misled and we continue asking for loans, which our grand grand children they haqve to come and pay!! Shame on us!!! We have to change.
   
 14. a

  andreakalima JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2016
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 2,917
  Likes Received: 1,809
  Trophy Points: 280
  Pongezi mwafrika halisi Ndugu Mo kwa nini usirudi nchini mwako ukachukua fomu ya kugombea urais?
   
Loading...