Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
MZEE BILAL REHANI WAIKELA AMELAZWA MOI GOROFA YA 2 CHUMBA NO 2 KITANDA NO. 5
Ndugu zangu leo asubuhi nimejaaliwa kwenda MOI kumjulia hali Mzee Waikela.
Nimemkuta macho na namshukuru Allah kwa hili kwani ningemkuta kalala nisingethubutu kumwamsha ingebidi niondoke.
Mzee wetu amepokelewa jana hapo hospitali akitokea Tabora.
Mzee Waikela ameanza kupata matibabu.
Mzee Waikela ana historia isiyo na mfano kwanza katika kuuendeleza mbele Uislam na pili katika kuunda chama cha TANU Western Province na kupigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Julius Nyerere na wazalendo wengine.
Mzee Waikela ni katika wazalendo wachache sana ambao wana historia ya kutukuka katika harakati za Uislam na katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Waikela alikuwa kiongozi ndani ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na alikuwa pia mstari wa mbele katika TANU.
Hivi sasa Mzee Waikela ni katika wanachama waasisi wa TANU wachache sana walio hai.
Na kwa hakika wazalendo hawa wanahesabika katika kiganja cha mkono.
Ndugu zangu katika kipindi hiki cha maradhi ya mzee wetu huyu tunahitaji tuwe pamoja katika kumsaidia kwa kila hali na kumuombea dua.