MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 710
Kuna habari mpya ambayo nimeinasa hivi punde kwenye wavuti wa Tanzania Daima, ambayo imechapishwa kwenye toleo la Ijumaa, 19 Julai 2013, yenye kichwa cha habari Bilal kuwaweka kitimoto watendaji Dar.
Ukisoma "kati kati ya mistari" ya habari hiyo, utagundua kuna utata mkubwa. Ngoja niwadadavulieni utata wenyewe ulipo:
Utata uliopo ni huo wa kutaja tarehe za ziara hiyo, kama alivyonukuliwa Waziri wa Nchi (OMR), Mazingira, Terezya Huviza. Kwa kuiweka hadharani ratiba hiyo, anawapa nafasi watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana kuweka safi maeneo tajwa, ili wakati wa ziara hiyo Makamu wa Rais asipate cha kuongea. Hii ni kum-sabotage Makamu wa Rais na kitendo hiki ni cha kulaaniwa, kwani Waziri Huviza yuko tayari kuwatetea watendaji wabovu na kuwalinda, ilhali Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri zake zikiendelea kukithiri kwa uchafu. Dar es Salaam iko kwenye kiwango cha jiji la 23 duniani kwa uchafu, kama ilivyoripotiwa na gazeti la New York Times, toleo la 1 Julai 2013, siku ambayo Rais Obama wa Marekani alipotua hapa nchini.
Huu ni uhuni uliokithiri kwani mbinu hii ya kutaja tarehe za ziara za viongozi imekuwa ikitumika kwa muda mrefu sasa, ili kuendelea kuwalinda wahusika. Ushauri wangu kwa Makamu wa Rais ni kuwachukulia hatua kali za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi, kuwachunguza kwa kuwaundia tume maalum, na hatimaye kuwashusha vyeo, kwani hatuwezi kuvumilia kuwa na watendaji wabovu kwenye halmashauri zetu, ambao wanachangia serikali kukosa mapato yake kutokana na idadi ya watalii kupungua kwa kuwa Jiji la Dar LINASIFIKA KIMATAIFA kwa UCHAFU!
Licha ya Huviza kusema kwamba "watendaji hao wamekuwa wagumu" akionekana kujikosha, hata yeye hajasimamia vizuri Wizara yake, na dhahiri ameonesha udhaifu mkubwa kwetu sote.
Mama Huviza, nilikuwa na matumaini makubwa nawe ulipoanza kazi. In fact, nilimsifu sana Rais alipokuteua, lakini umedhihirisha udhaifu wako katika utendaji. Nawe unabeba lawama kutokana na uchafu uliokithiri hapa Dar. Tumechoka kuziba pua zetu tukipita mitaani, kwenye madampo yasiyo rasmi, yenye uvundo wa wiki na miezi.
Bora ung'atuke KABLA hujang'atuliwa!

Halmashauri wamekuwa wagumu kuitikia agizo la makamu wa rais, ndiyo maana anafanya hii ziara ili wamweleze sababu ya kutoitikia, alisema Dk. Huvisa na kuongeza kuwa kiongozi huyo atatembelea maeneo kadhaa ya jiji pamoja na Mkoa wa Pwani.
Alisema Julai 21 atatembelea Soko la Buguruni kuona hali ya usafi, uwanja wa ndege, eneo la Pugu Dampo, Mbagala Mwisho, Machinga Complex, eneo la kwa Mwalimu Nyerere, Tanganyika Packers, Mwenge na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Alisema Julai 22 atatembelea eneo la Jangwani, Tandale Sokoni, Soko la Mabibo, Kigogo, Tabata Dampo, Ubungo, Kimara, Tegeta, Wazo na Bagamoyo na kisha baadaye kufanya mkutano wa watendaji ili kuzungumza nao mambo mbalimbali.