chazachaza
JF-Expert Member
- Feb 21, 2018
- 2,829
- 3,825
Habari za wasaa WanaJF,
Poleni na yanayoendelea nchini, lakini tusuvunjike moyo yatapita,hakuna lisilo kuwa na kikomo.
Niende moja kwa moja kwenye mada.
AFRICA ndio bara pekee lililobatizwa majina mengi.Dunia inalitambua bara la Africa kwa majina mengi ya ajabu ajabu na kukatisha tamaa!! Mara the poorest continent ,the continent with selfish leaders n.k
Majina haya hatukuyabuni sisi wa Africa,Bali tulibatizwa na wale wanaojiita majina mazuri mazuri na yenye mvuto ,akina developed nation,upper economic countries, G7,elite countries, supper power countries n.k nadhani Africa ilipachikwa haya majina kwa makusidi maalum,na kwa bahati mbaya haya majina yakapenya kwenye bongo za waafrica na yakakubalika kwa mikono miwili na wasomi wetu,watoto wetu na wajukuu wetu.
Cha ajabu majina haya yamesadifu na kubeba vinasaba vya waafrica.Nadhani kale kamsemo kanachosema majina hubeba hatimana muonekano wa mtu si kakukapuuza kabisaaa! na kale kanakosema ukitaka kummaliza adui mdogomdogo usisumbuke kutumia nguvu Kwanza!, Mbatize jina baya tu, inatosha.haka kamsemo nako sikakubeza kabisaaa!
lakini ukitafakali kwa akili za kizalendo za akina kwame nkurumah,nyerere,gadafi,magufuli n.k utapata majibu tofauti na utastaajabu kiasi gani heshima na utu wa Africa unavyofitinisha.
Ndio,heshima ya Africa inafitinishwa.
Wachina Hawa ambao kwa Sasa wameenea kalibia Africa yote,bila kubisha Africa ni Kama roho yao na pumzi yao kwa Sasa.africa imebeba ajira maelfu kwa maelfu za wachina, China ya leo inang'aa kwa sababu ya uwepo wa sisi tuliopewa majina mabaya mabaya na ya zarau,wanatuita poorest continent je hivi mtu maskini anaweza kumuajiri tajiri!!?? bila Shaka jibu ni hapana,Sasa kwa nn walitubatiza haya majina ya dharau ili hali sisi ndo tunafanya waonekane Kama waonekanavyo leo!?
Nguvu ya China leo inatoka Africa,uhai wa viwanda vya China leo unatoka Africa na upo Africa,hii midharau ya kuitana majina mabaya inatoka wapi!? Kwa sababu ya uwepo wa Africa China Sasa inapaa kiuchumi, China Sasa inapaa ki technology,China Sasa imekuwa threat kubwa kwa mmarekani na dunia yote,hii yote ni Africa imemuweka kwenye ramani.
Wamalekani Hawa ndo waliogundua miaka hiyo nguvu na kiburi Cha German kilitoka wapi,jibu walipata Africa .Kama kawaida yao walipogundua hawakumpa nafasi tena German kuotesha mizizi Africa ,na nikweli ujerumani ilipotoa miguu Africa na yenyewe ikapoteana Hadi leo,uingereza nayo hivyohivyo,je hizi dharau za kuitana majina mabaya mabaya zinatoka wapi!?
kwa Sasa mmarekani na mchina ndo mataifa yanayo hasimiana kiuchumi,kuhasimiana kwao tunaumia sisi,sisi ambao tumewafikisha hapo walipo.siku Africa ikatokea imehamia sayari ya mars na kila kitu ilicho nacho ninauhakika.
Marekani, China,Ujerumani,Ufaransa,Japan,Uingereza, Italy wote wataunga tela waje pia mars. na huenda ikawa nchi zote zikaunga tela kuifuata Africa sayari ya mars.pengine watakao komaa kubaki ni wale ndugu zangu wa Korea kazkazini,maana yule bwana kwa misimamo yake ,sidhani Kama wataweza kuchomoka.
Wakati mwingine huwa nawashangaa baadhi ya wasomi wetu ,ambao husema bila aibu eti , Africa inatunzwa na wazungu,nawashangaa Sana,au ni yale majina ya ajabu ajabu tuliyobatizwa yamewakaa vilivyo kwenye medula oblangata zao!! Wanashindwa kujua bila uwepo wa Afrika hakuna Marekani yenye nguvu, hakuna China yenye nguvu.!!!
Note; This is the first topic for me to post here JF. Tusameheane kwa mwandiko.
Nawasilishwa; Karibuni kwa mjadala.