Bila uwepo wa Afrika hakuna Marekani yenye nguvu, hakuna China yenye nguvu

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
2,829
3,824
Habari za wasaa WanaJF,

Poleni na yanayoendelea nchini, lakini tusuvunjike moyo yatapita,hakuna lisilo kuwa na kikomo.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

AFRICA ndio bara pekee lililobatizwa majina mengi.Dunia inalitambua bara la Africa kwa majina mengi ya ajabu ajabu na kukatisha tamaa!! Mara the poorest continent ,the continent with selfish leaders n.k

Majina haya hatukuyabuni sisi wa Africa,Bali tulibatizwa na wale wanaojiita majina mazuri mazuri na yenye mvuto ,akina developed nation,upper economic countries, G7,elite countries, supper power countries n.k nadhani Africa ilipachikwa haya majina kwa makusidi maalum,na kwa bahati mbaya haya majina yakapenya kwenye bongo za waafrica na yakakubalika kwa mikono miwili na wasomi wetu,watoto wetu na wajukuu wetu.

Cha ajabu majina haya yamesadifu na kubeba vinasaba vya waafrica.Nadhani kale kamsemo kanachosema majina hubeba hatimana muonekano wa mtu si kakukapuuza kabisaaa! na kale kanakosema ukitaka kummaliza adui mdogomdogo usisumbuke kutumia nguvu Kwanza!, Mbatize jina baya tu, inatosha.haka kamsemo nako sikakubeza kabisaaa!

lakini ukitafakali kwa akili za kizalendo za akina kwame nkurumah,nyerere,gadafi,magufuli n.k utapata majibu tofauti na utastaajabu kiasi gani heshima na utu wa Africa unavyofitinisha.

Ndio,heshima ya Africa inafitinishwa.

Wachina Hawa ambao kwa Sasa wameenea kalibia Africa yote,bila kubisha Africa ni Kama roho yao na pumzi yao kwa Sasa.africa imebeba ajira maelfu kwa maelfu za wachina, China ya leo inang'aa kwa sababu ya uwepo wa sisi tuliopewa majina mabaya mabaya na ya zarau,wanatuita poorest continent je hivi mtu maskini anaweza kumuajiri tajiri!!?? bila Shaka jibu ni hapana,Sasa kwa nn walitubatiza haya majina ya dharau ili hali sisi ndo tunafanya waonekane Kama waonekanavyo leo!?

Nguvu ya China leo inatoka Africa,uhai wa viwanda vya China leo unatoka Africa na upo Africa,hii midharau ya kuitana majina mabaya inatoka wapi!? Kwa sababu ya uwepo wa Africa China Sasa inapaa kiuchumi, China Sasa inapaa ki technology,China Sasa imekuwa threat kubwa kwa mmarekani na dunia yote,hii yote ni Africa imemuweka kwenye ramani.

Wamalekani Hawa ndo waliogundua miaka hiyo nguvu na kiburi Cha German kilitoka wapi,jibu walipata Africa .Kama kawaida yao walipogundua hawakumpa nafasi tena German kuotesha mizizi Africa ,na nikweli ujerumani ilipotoa miguu Africa na yenyewe ikapoteana Hadi leo,uingereza nayo hivyohivyo,je hizi dharau za kuitana majina mabaya mabaya zinatoka wapi!?

kwa Sasa mmarekani na mchina ndo mataifa yanayo hasimiana kiuchumi,kuhasimiana kwao tunaumia sisi,sisi ambao tumewafikisha hapo walipo.siku Africa ikatokea imehamia sayari ya mars na kila kitu ilicho nacho ninauhakika.

Marekani, China,Ujerumani,Ufaransa,Japan,Uingereza, Italy wote wataunga tela waje pia mars. na huenda ikawa nchi zote zikaunga tela kuifuata Africa sayari ya mars.pengine watakao komaa kubaki ni wale ndugu zangu wa Korea kazkazini,maana yule bwana kwa misimamo yake ,sidhani Kama wataweza kuchomoka.

Wakati mwingine huwa nawashangaa baadhi ya wasomi wetu ,ambao husema bila aibu eti , Africa inatunzwa na wazungu,nawashangaa Sana,au ni yale majina ya ajabu ajabu tuliyobatizwa yamewakaa vilivyo kwenye medula oblangata zao!! Wanashindwa kujua bila uwepo wa Afrika hakuna Marekani yenye nguvu, hakuna China yenye nguvu.!!!

Note; This is the first topic for me to post here JF. Tusameheane kwa mwandiko.

Nawasilishwa; Karibuni kwa mjadala.
 
Kuna dini kabisa zinadiliki kusema taifa fulani fulani huko ndio matukufu alafu Afrika :ngozi nyeusi imelaaniwa: Nayashangaaga sana haya madini ya hovyo namna hii.

Alafu utakuta lijamaa la Afrika lanayapigania haya madini lipo tayari hata kufirisika au kufa kabisa.
 
Wakati mwingine huwa nawashangaa baadhi ya wasomi wetu ,ambao husema bila aibu eti , Africa inatunzwa na wazungu,nawashangaa Sana,au ni yale majina ya ajabu ajabu tuliyobatizwa yamewakaa vilivyo kwenye medula oblangata zao!! Wanashindwa kujua bila uwepo wa Afrika hakuna Marekani yenye nguvu, hakuna China yenye nguvu.!!!
Hata kama itakuwa ulichokiandika ni kweli.
Kwamba africa ndio chanzo cha china na marekani kuwa juu.

Je unadhani hiyo itaondoa ukweli na uhalisia kwamba africa ni
Tegemezi.
Masikini.
Viongozi hafifu.
Nk....

Na majina yote ambayo unasema tumepewa japo kiuhalisia ndio ukweli wenyewe ambao ni mchungu.

Unadhani hiyo itabadilisha uhalisia?
 
namba 3 nakubali.na ndo kinachozalisha namba 1.namba 2 sio kweli.
 
Ni Kweli without Africa hakuna maendeleo Ulaya au USA.

Wametutumia sisi Waafrika kama milioni moja kwa miaka 400. Kujenga (white house), majengo yote ya kifahari, kulima, kufanya shughuli za kila aina.

Ina majina mengi moja ni Ethiopia, Kemet, Alkebulan.
 
punguza jazba mkuu.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Sio jazba ndugu ujuwe ni kweli wazungu hawapendi kuona nchi za Africa zenye utajili zikiutumia utzjiliwake kwa maendeleo na ndoma unaona kama Congo,Libya..watawachonganisha wenyewe kwa wenyewe mpaka msijitawale lakini tatzo kubwa ni hawa vongozi wetu...Mtu akishakaa juu pale anajiona ye ndo anaakili kupita wote alafu nawe unakuja kuwataja baadhi yao kwenye kundi la wazalendo..
 
Hivi likatokea janga, Dar yote ikawa flat hakuna cha kiwanda, bandari wala K'koo, au CHEDEMA waasi wakaikamata Dar😴. Serikali ikakimbilia Dom. Nacho taka kuuliza hivi bila Dar Taifa litaweza kusonga mbele?
 
Habari za wasaa WanaJF,

Poleni na yanayoendelea nchini,lakini tusuvunjike moyo yatapita,hakuna lisilo kuwa na kikomo.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

AFRICA ndio bara pekee lililobatizwa majina mengi.Dunia inalitambua bara la Africa kwa majina mengi ya ajabu ajabu na kukatisha tamaa!! Mara the poorest continent ,the continent with selfish leaders n.k

Majina haya hatukuyabuni sisi wa Africa,Bali tulibatizwa na wale wanaojiita majina mazuri mazuri na yenye mvuto ,akina developed nation,upper economic countries,G7,elite countries, supper power countries n.k nadhani Africa ilipachikwa haya majina kwa makusidi maalum,na kwa bahati mbaya haya majina yakapenya kwenye bongo za waafrica na yakakubalika kwa mikono miwili na wasomi wetu,watoto wetu na wajukuu wetu.

Cha ajabu majina haya yamesadifu na kubeba vinasaba vya waafrica.Nadhani kale kamsemo kanachosema majina hubeba hatimana muonekano wa mtu si kakukapuuza kabisaaa! na kale kanakosema ukitaka kummaliza adui mdogomdogo usisumbuke kutumia nguvu Kwanza!, Mbatize jina baya tu,inatosha.haka kamsemo nako sikakubeza kabisaaa!

lakini ukitafakali kwa akili za kizalendo za akina kwame nkurumah,nyerere,gadafi,magufuli n.k utapata majibu tofauti na utastaajabu kiasi gani heshima na utu wa Africa unavyofitinisha.

Ndio,heshima ya Africa inafitinishwa.

Wachina Hawa ambao kwa Sasa wameenea kalibia Africa yote,bila kubisha Africa ni Kama roho yao na pumzi yao kwa Sasa.africa imebeba ajira maelfu kwa maelfu za wachina,China ya leo inang'aa kwa sababu ya uwepo wa sisi tuliopewa majina mabaya mabaya na ya zarau,wanatuita poorest continent je hivi mtu maskini anaweza kumuajiri tajiri!!?? bila Shaka jibu ni hapana,Sasa kwa nn walitubatiza haya majina ya dharau ili hali sisi ndo tunafanya waonekane Kama waonekanavyo leo!?

Nguvu ya China leo inatoka Africa,uhai wa viwanda vya China leo unatoka Africa na upo Africa,hii midharau ya kuitana majina mabaya inatoka wapi!? Kwa sababu ya uwepo wa Africa China Sasa inapaa kiuchumi,China Sasa inapaa ki technology,China Sasa imekuwa threat kubwa kwa mmarekani na dunia yote,hii yote ni Africa imemuweka kwenye ramani.

Wamalekani Hawa ndo waliogundua miaka hiyo nguvu na kiburi Cha German kilitoka wapi,jibu walipata Africa .Kama kawaida yao walipogundua hawakumpa nafasi tena German kuotesha mizizi Africa ,na nikweli ujerumani ilipotoa miguu Africa na yenyewe ikapoteana Hadi leo,uingereza nayo hivyohivyo,je hizi dharau za kuitana majina mabaya mabaya zinatoka wapi!?

kwa Sasa mmarekani na mchina ndo mataifa yanayo hasimiana kiuchumi,kuhasimiana kwao tunaumia sisi,sisi ambao tumewafikisha hapo walipo.siku Africa ikatokea imehamia sayari ya mars na kila kitu ilicho nacho ninauhakika ,Marekani,China,Ujerumani,Ufaransa,Japan,Uingereza, Italy wote wataunga tela waje pia mars. na huenda ikawa nchi zote zikaunga tela kuifuata Africa sayari ya mars.pengine watakao komaa kubaki ni wale ndugu zangu wa Korea kazkazini,maana yule bwana kwa misimamo yake ,sidhani Kama wataweza kuchomoka.

Wakati mwingine huwa nawashangaa baadhi ya wasomi wetu ,ambao husema bila aibu eti , Africa inatunzwa na wazungu,nawashangaa Sana,au ni yale majina ya ajabu ajabu tuliyobatizwa yamewakaa vilivyo kwenye medula oblangata zao!! Wanashindwa kujua bila uwepo wa Afrika hakuna Marekani yenye nguvu, hakuna China yenye nguvu.!!!

Note; This is the first topic for me to post here JF. Tusameheane kwa mwandiko.

Nawasilishwa; Karibuni kwa mjadala.
Hongera kwa hoja isiyojadilika
 
Magufuli wa chato anauzalendo gani?

Kuna vitu amefanya vizuri sana, miundombinu, hospitali, barabara, umeme, nidhamu, rushwa, shule, vyu.

Kuwaambia Watanzania wajiamini, kwamba hatuna mjomba wala shangazi. Tuipiganie nchi sisi wenyewe. Hakuna watu wanaotupenda sana. Huu ni uzalendo.

Anakosea hapa na pale. Hotuba muhimu ziandikwe na kusomwa.
 
Umeshaambiwa hii miradi ya magufuli ni tembo mweupe, ndiyo chaka lao la kupigia Ela, amedabo deni la taifa, hajaongeza mishahara tokea aingie madarakani, biashara zinapumulia mashine, magufuli ni mzalendo kwa chato siyo Tanzania
 
@TIASA
Barabara huzioni? Umeme ulikuwa unakatika kila siku, maji yalikuwa tatizo, elimu bure, Watoto wapya milioni mbili over 10 watoto milioni 20.

Huduma za serikali uzembe, umepungua.
Unanijua mimi ni nani, imeisha.

Uzalendo ni nini?

Ufanye nini kuitwa mzalendo? ( mtu anayejali nchi yake, watu wake)
 
Back
Top Bottom