kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,793
- 5,053
Kuna mwanamke mmoja hivi X wangu ambaye nilikuwa napambana sana arudi, na kwa bahati nzuri nilifanikiwa kumrudisha. Kumbe alikuwa anarudi kwa faida zake mwenyewe!
Yaani tulikuwa bado tuna wiki mbili tu toka turudiane, akaniambia babe nina tatizo naomba unikopee pesa kwa ndugu yako fulani hivi, eti atarudisha mwezi wa kumi 12. Nikaamuliza ngapi? Eti milioni 2, si kushangaa maana yeye ni mfanya biashara na ana uwezo wa kurudisha pesa hizo.
Ila kilichonipa ugumu ni kuwa, mimi ni sina chochote na ndugu yangu huyo hawezi kunikopa pesa kwasababu anajua sina shughuli yeyote mjini hapa, na pia nikafikiria, Tanzania hii unaweza kwenda kumkopea mtu mwisho wa mwezi akakugeuka.
Nikamwambia babe siwezi kabisa na sidhani kama ndugu yangu anaweza kunikopesha pesa hizo. Bora uende mwenyewe, maana anakujua wewe ni mfanya biashara, hawezi kukunyima akiwa nazo.
Alichokuja kuniambia, eti pumbavu tafuta pesa, nilitaka nikuingize matatizo ili uache upumbavu! Wenzako wanatafuta pesa, kazi yako ni kubeti Jumatatu hadi Jumapili!