Bila mpatanishi (Mediator), hakuna muafaka kati ya CCM na CHADEMA

Ina maana muafaka waliofikia Ccm na Cdm huna imani nao ?


..kuna mazungumzo yanaendelea.

..hakuna muafaka ambao umefikiwa.

..muafaka hufikiwa wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya maridhiano.

..mimi kwa upande wangu naamini tunahitaji kuunda Tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano, ambayo itaangazia masuala ya uvunjwaji wa haki uliofanywa na vyombo vya dola na mahakama.
 
Hoja nzuri. CHADEMA wameingia kwenye maridhiano kinyonge sana wakati walikuwa kwenye upande wenye nguvu sana ukizingatia hali ya siasa ndani ya CCM baada ya kifo cha Magufuli. Watapotezewa muda ili CCM wajipange zaidi kisiasa halafu majadiliano yatavunjika.

Niliwahi kuleta mada inayofanana na hii mwaka 2018:

Njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani ni hii
 
Mbowe ataongezewa Sega jingine lenye asali anyamaze.
Sasa hv ni mwendo wa masega tu yaliyojaa asali,na mwendo wa kumsifia mama,alafu unakuwa na vibe la kinafiki wafuasi wako hasa wale ambao ni slow learners ambao ndio wengi Tanzania ya leo wanaona umewasha moto balaa kumbe ww unaujua mchezo mlioridhiana,ila wenye Akili ambao ni wachache wanatulia tu wanaona jinsi slow learners wanavyotoa bovu kwa mavibe ya kinafiki kutoka kwa viongozi wasijue kwamba masega yaliyojaa asali yalishaliwa zamani.Kazi tunayo ndugu zangu.Mambo yanaumiza sana nchi hii basi tu.
 
Back
Top Bottom