Bila Kadi kwa mtu mzima hupandi mwendokasi

Bila Kadi kwa mtu mzima hupandi mwendokasi

Kuanzia leo Julai 1, 2025, huduma ya Mabasi ya Mwendokasi jijini Dar es Salaam imesitisha rasmi matumizi ya tiketi za karatasi kwa abiria wa kawaida na kuanza kutumia mfumo wa kadi maalum zenye salio.

Abiria sasa wanatakiwa kuwa na kadi hizo, zitakazopatikana katika kwa shilingi elfu moja na kujazwa salio katika vituo mbalimbali vilivyokuwa vikitoa tiketi.

Hali hiyo imeibua mtazamo tofauti kwa baadhi ya abiria, hususan maeneo ya Morogoro Road, ambao wamedai hawakufahamu kuhusu mabadiliko hayo mapya. Wengine wamesema mfumo huo mpya unaweza kuwa changamoto kwa wananchi wa kipato cha chini.

Wafanyakazi wa vituo vya Mwendokasi wameeleza kuwa tiketi za karatasi zitaendelea kutumika kwa wanafunzi pekee. Vituo kama Mbezi Mwisho, Kibanda cha Mkaa, Kwa Msuguli, Temboni, Suka na Stop Over vimewekewa mashine maalum za kuskani kadi.
Kadi itapunguza ufisadi.
Sasa huyo mwananchi anayelalamika matumizi ya kadi
Itakuwa hawajawi kukutana na kero za kupanga foleni kukata tiketi vituo vyenye watu wengi sana.

Atafute elfu 10 aweke
Kama nauli anaweza kupata basi hata ya kuweka kwenye kadi hawezi kukosa.
Kama akikosa kabisa
Ni simple,anamuomba mtu mwenyw kadi amvushe kwa kumpatia nauli yake mwenye kadi.
 
Hili wazo lako nimeliwaza na kuliwazua,huenda kuna watu ndio itakuwa biashara yao iyo mtu mjanja anakuwa na salio la kutosha kisha anakaa nje ya geti kwa wale wasiokuwa na kadi itawalazimu kumpatia mtu buku anamfungulia kisha unapita zako,kwaiyo fursa iyo kwa wale wajanja nimeiona labda itokee wenye mamlaka waizuie
 
Pale feri walinzi wanamiliki kadi na anaakuvusha kwa miatano siku ambayo umesahau kadi.
Au unapitia ule mlango wao ambao hauna sehemu ya kuscan Kwahiyo kila sehemu ni fursa.
Naiua ni uvunjifu wa sheria ila inatusaidia mara mojamoja.

Japo abiria wengi hawana muda wa kufanya hiyo biashara. Wengi unamcopansate tu na amount inayotakiwa anakuvusha.
 
Back
Top Bottom