Bila agenda ya wafanyakazi kazi ya wafanyabiashara na wakulima itasuasua

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,307
12,604
Wafanyabiashara, wakulima na wajasiliamali agenda yao inafanyiwa kazi mara Kwa mara, mikutano ya kusikiliza kero zao ni mara Kwa mara, na wanaozorotesha biashara zao wanatimuliwa. Ila agenda ya wafanyakazi na kero zao agharabu zinapatitiwa majibu ya haraka. Wafanyakazi wanalipa kodi nyingi Sana pamoja na kulipa hadi 30% ya mapato Yao. Ukishalipa PAYE bado kodi nyingine kama VAT na kodi nyingine zote zinakuhusu.

Mfanyakazi ndiye mkusanyakodi, mlinzi, hakimu, mwalimu, muuguzi, tabibu na dereva, mchimbaji migodini, nk. Mfanyakazi mwenye njaa hawezi kuwa mkusanya kodi,mlinzi, hakimu, mwalimu, tabibu au dereva mzuri. Hata ukimchinja atafanya kila kitu hapohapo anapofanyakazi ili kupata chakula, malazi, mavazi, karo ya shule, matibabu, pombe yake, mchango wa harusi, nauli, na kuwasaidia watoto wa dada yake wenye shida popote walipo.
Tabia halisi ya mfanyakazi mwenye kipato kidogo ni wizi, rushwa, utoro, uwongo, hasira, kufanyakazi kigoigoi, kupiga umbea,na kukata tamaa. Huyu hawezi kumhudumia vizuri mfanyabiasha, mkulima, na mvuvi watakapo hitaji huduma take.

Tuanze kutatua kero za wafanyakazi kabla ya kutatua zile za wafanyabiashara na wakulima vinginevyo tutatengeneza vicious cycle kiuchumi.

Tuangalie kero za wafanyakazi Kwanza kwakuwa wao ndio watakaowahudumia wafanyabiashara, wakulima, wafugani, wavuvi.
 
Back
Top Bottom