Msigazi Mkulu
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 4,137
- 3,323
Katika hali isiyo ya kawaida, watumishi wa idara ya elimu( waalimu) walioajiriwa mwaka jana, wameitwa na mkurugenzi wa halmashauri ili kurudisha pesa zilizoongezeka mwezi wa tatu. Ikumbukwe mwezi huo wa tatu watumishi wengi walilipwa madeni yao hasa ya mishahara.
Kuna watumishi tuliowekewa pesa wakati hatudai yaani mshaara wa mwezi wa tatu ulikuwa doubled. Hii ni kwa nchi nzima. Cha kusikitisha leo tumeitwa na mkurugenzi ili turudishe hizo pesa za mshaara mmoja. Alikuwepo pia afisa wa TAKUKURU ambaye ametwambia ni kosa kisheria kuchukua pesa ambazo zimeongezeka bila kuwa halali.
Sisi hatujagoma kurudisha japo tunaumia sana maana tutakuwa na hali ngumu mwezi ujao lakini tuna wasiwasi kwa namna zitakavyo rejeshwa maana tumeambiwa tunazipeleka kwa mwasibu wa halimashauri.
Hapo si zitapigwa na wajanja wa halmashauri kweli. Kwa nini mkurugenzi asipeleke majina yetu hazina wakatukata hukohuko?
Wajuzi wa haya mambo naomba mtwambie kitu.