Bifu la song na eto'o sasa lafikia patamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bifu la song na eto'o sasa lafikia patamu

Discussion in 'Sports' started by baraka boki, Jun 4, 2011.

 1. b

  baraka boki Senior Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, amekutana na viongozi watatu wa chama hicho wanaotuhumiwa kwa ufisadi, katika utekelezaji wa uamuzi wa kujivua gamba uliofanywa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) uliofanyika Dodoma Aprili 10 hadi 11, mwaka huu.

  Yaliyozungumzwa katika kikao hicho yameelezwa kuwa siri kati ya Msekwa na watuhumiwa hao, Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, lakini yalihusu agizo walilopewa watafakari, wajipime na kuchukua hatua wao wenyewe kwa masilahi ya CCM, la sivyo wawajibishwe na chama.

  Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM mjini Dar es Salaam, ilisema Msekwa
  alikutana na viongozi hao kila mmoja kwa wakati wake na kuzungumza nao kwa faragha kama Makamu Mwenyekiti wa CCM na kama mzee wa chama hicho.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Msekwa alikutana na viongozi hao Mei 26 mwaka huu na wa kwanza alikuwa Rostam ambaye ni Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Igunga. Walikutana saa 2.30 asubuhi.

  Baada ya hapo kwa mujibu wa taarifa hiyo, alifuata Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu, Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC na wa mwisho alikuwa Chenge, Mjumbe wa NEC na Mbunge wa Bariadi Magharibi.

  “Kwa vile Msekwa alikutana kwa faragha na viongozi hao mmoja mmoja, anayejua kilichozungumzwa ni Mzee Msekwa na wao peke yao,” ilisema taarifa hiyo ya CCM.

  Gazeti hili lilizungumza na Lowassa, kutaka kujua kama alikutana na Msekwa na kama atachukua uamuzi wa kujivua gamba kama maagizo ya NEC yanavyotaka lakini baada ya kusikiliza hoja hizo, alijibu “No comment.”

  Alipotafutwa Rostam, simu yake ilipokewa na msaidizi wake ambaye hakutaka kujitambulisha
  jina, akasema Mbunge huyo yuko nje ya nchi na ameacha simu kwake. Chenge simu yake iliita bila majibu.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua itakayofuata baada ya mazungumzo hayo ni kufikisha
  kwenye vikao vya CCM taarifa ya mambo yaliyojiri wakati wa mazungumzo hayo na vikao hivyo vitatoa uamuzi utakaotangazwa kwa umma.

  CCM pia imekanusha taarifa kwamba viongozi hao walipokutana na Msekwa walikabidhiwa
  barua za kuwataka wajiuzulu na zile zilizodai kuwa barua hizo zimefungiwa kabatini na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete.

  “Taarifa zote hizo zilizoandikwa na kutangazwa katika vyombo vya habari, si za kweli, ni uongo na uzushi mtupu. Hakuna barua iliyoandikwa, hakuna aliyepewa barua na wala hakuna barua iliyofungiwa kabatini,” ilifafanua taarifa hiyo.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Bw mkubwa, sielewi song & eto'o wanavyohusiwhwa na habari hii. au eto'o/song = msekwa? kikwete? /magamba 3 (lowassa & co.) kivipi?
   
 3. Iramusm

  Iramusm JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 424
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  hii kali!
   
 4. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  hii heading na habari ndani vinaendana kweli kamanda? mana ina-mix kwelikweli!!!
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Duh GT.com
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ha ha ha...hizi Copy & Paste kuna watu zinawapelekesha kubaya! LOL...hillarious!
   
 7. T

  The Priest JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huna mpya,acha ushabiki.
   
 8. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Du! Tuko kwenye sports, jamaa anatupiga siasa
   
Loading...