Naomba Kusema Ukweli huu na Bahati Nzuri Jose ni Mtu Wangu wa Karibu Sana na Juzi Nilikuwa Nimekaa Nae VIP B Wakati wa Mechi Yetu na Rhino na Jana Pia Jumatatu Nilifanya Nae Mazungumzo na Kiujumla Wadau Owino Alifunguka Sana Kwangu Kuhusiana na Mzozo Wake na Loga na Nikimnukuu Alisema Kwamba Tatizo ni Tabia Ya Kocha Kumtukana Matusi tena Yale Ya Nguoni na Pia Owino Anapinga Kitendo cha Loga Kuwatoa Hovyo Wachezaji na Amekilaani Sana ila Nilichompendea Owino Kiukweli ni Kukiri Kuwa Loga ni Kocha Mzuri Sana Ila Ana Tatizo la Jazba au Hasira. Alichioniambia ni Kuwa Viongozi Wanalishughulikia hilo Suala ila Inaonekana Kocha Hajaridhishwa na Kitendo cha Owino Kugomea ama Kususa Mazoezi na Pia Alichelewa Kurudi Kwao Kujiunga na Wenzake ktk Kambi. Nitaendelea Kuwajuza Kadri Nitakavyokuwa Nawasiliana na Joseph Owino Gera Kuhusiana na Sakata Lake na Loga ila Kwa Simba Kukosekana Kwake ni Pengo Kubwa Mno na Kwa Mlioingia Uwanjani Juzi Mliona Na Ilikuwa ni Tia maji Tia maji na Donald Mosoti Alituokoa Sana Vinginevyo Vitini Kulikuwa Hakukaliki.
Huu ni mgongano wa kocha mwenye msimamo dhidi ya mchezaji mwenye msimamo. Ufumbuzi wake unahitaji uongozi wenye msimamo ambao sina hakika kama unapatikana kwenye Simba iliyopo. Matokeo yake yanaweza kuwa na hatari kwa Simba. Akishinda Owino, wachezaji wenzake watapata funzo la kumdindia kocha wao anayeonekana kama mwenye mbinu za ki Al Qaeda hivi. Akishinda kocha, ataelekeza tabia hiyo kwa wengine, kwa kuanza na Mwombeki.
Kwa mujibu wa baadhi ya magazeti, Simba iko tayari kuachana na Owino kulko kuachana na kocha. Lakini waangaliesana, wanidanganyike na ushindi wa Mtani Jembe. Siku Simba ikifungwa kwenye mechi ya ligi, kocha wa aina hii ataanza kutukana wachezaji, viongozi mpaka washabiki!Simba ikiwa na msimamo itaelewa Owino is one of the best player "beki" namba moja Simba, kukosekana kwa Owino kunai cost team ile mbaya.. Mpaka wachezaji wanamuogopa kocha sasa hivi.
Jamani!jamani nyie acheni uongo,mbona nasikia tatizo ni "MADAGAA" bhana?
Cc Masuke