Biden atoa ahadi ya kuwaondoa raia wake Afghanistan

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Rais wa Marekani Joe Biden ameapa kuwa atawarejesha nyumbani raia wote wa Marekani kutoka nchini Afghanistan pamoja na Waafghani waliosaidia juhudi za nchi yake kwenye vita vya karibu miaka 20.

Biden ametoa ahadi hiyo alipozungumza na waandishi habari mjini Washington wakati hatma ya maelfu ya Wamarekani waliokwama kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul bado haijulikani.

Hadi kufikia sasa ni watu 5,700 pekee ikiwemo Wamarekani 250 ndiyo wameondoshwa nchini Afghanistan na kupelekwa kwenye vituo vya muda vilivyoandaliwa kwenye mataifa jirani.

Utawala wa Biden unaandamwa na ukosoaji mkubwa nyumbani kutokana na kuchukua hatua za polepole za kuwahamisha raia wake tangu kundi la Taliban lilipoukamata mji mkuu wa Afghanistan, Kabul siku kadhaa zilizopita.
 
Kuna mziki utawaka hapo waajabu dunia itabakia kushangaa yanayotokea walai, hawa wakubwa hawaaminiki kabisa wnachokisema machoni sio wanachokipanga wajua kila kitu hawa.
 
Back
Top Bottom