Biden atashinda, Trump is done

Facts.

1. Trump na Biden hawana athari yoyote ile katika maisha yangu.

2. Hujui nilipo. Hivyo habari za deportation ni njozi zako tu.

3. Read and weep.
Uko Georgia. Ombea Biden ashinde maana Trump hana mzaha na wahamiaji kama nyie
 
Man, unachosema kipo popote pale duniani, na hii inategemeana na ukubwa + population ya maeneo husika na sio mfumo!!

CA, TX, FL, NY, IL, PA tangia hapo ni majimbo makubwa in terms of land size and population, na uwingi wa electoral colleges unabebwa na hilo suala and not otherwise!!

Na ingawaje ni kweli hata ukishinda CA, TX, FL na NY hawakupi ushindi lakini unakuwa katika NAFASI KUBWA ya kushinda! Kinyume chake, ukishindwa kwenye hayo majimbo unakuwa kwenye nafasi kubwa ya KUSHINDWA uchaguzi mzima!!!

Ni kama TZ tu, ukishindwa Kanda ya Ziwa na Dar es salaam, basi unakuwa kwenye hatari kubwa ya KUSHINDWA uchaguzi mzima na kinyume chake, unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kushinda!!!
 
Sijui wenzetu muishio USA mmejipangaje
Sisi huku kwetu UCHAGUZI UMEISHA! UCHAGUZI UMEISHA!!! UCHAGUZI UMEISHA!!!!!
Your browser is not able to display this video.
 
Sijui wenzetu muishio USA mmejipangaje
Sisi huku kwetu UCHAGUZI UMEISHA! UCHAGUZI UMEISHA!!! UCHAGUZI UMEISHA!!!!!
View attachment 1620544
Chaguzi karibu zote, huwa zina makandokando.

Mshindwa mara nyingi huwa anadai kaibiwa kura.

Hillary Clinton alidai kaibiwa kura na Urusi🤣🤣

Al Gore alidai kaibiwa kura na G. W. Bush.

Trump naye anadai anafanyiwa figisu.

Wale wa kwetu nao kila uchaguzi huwa wanalia kuibiwa kura.

Kwa ufupi, siasa ndivyo zilivyo.

Ni chaguzi chache sana zisizokuwa na figisu.

Uzuri ni kwamba, hawa wanasiasa, kwa kiasi kikubwa, huwa hawana athari za moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.

La muhimu kuliko yote, ni wewe kutokuwekeza hisia zako, furaha yako, akili yako, malengo yako, na matamanio yako kwa hao wanasiasa.

Presidents are temporary. Wu-Tang is forever!
 
CA na NY siyo miaka yote ni blue.

Au labda nikuulize, umeanza kuzifuatilia lini chaguzi za Marekani?

Manake mimi nakumbuka kuna landslides za watu kushinda majimbo 40, 44, na 49 kati ya 50!

Na baadhi ya majimbo waliyoshinda ni CA na NY.
CA toka walibadilika toka 1990 mpaka leo kutoka red kwenda blue imekuwa kama uhakika wa Democratic huwa inabadilika na ikitokea inakuwa ushindi wa kishindo kwa Rep kama wakati wa Reagan. kwa NY katika chaguzi 12 za mwisho Rep ni mara tatu tu kwa hiyo katika hali ya sasa zinaonekana ni stronghold za Dem hata mwaka huu Rep wametupwa mbali sana CA. Ila sisemi kuwa hazibadiliki na ikitokea basi kuna jambo kubwa linakuwa limetokea mara nyingi uchumi ukienda vibaya wanabadilika. kwa sasa kwa miaka mingi ni Democratic kama nyumbani.
 
Tunakubaliana kwa mengi lakini kusema kuwa kipo kokote duniani hapo tunatofautiana. NY sio kubwa kwa size lakini wana 29 votes wakati Nevada ni kubwa kwa size lakini wana 6 wao ni population ndio inaamua. Sasa kwa mfano uliotoa Tanzania kwa kuwa mfumo wetu ni kura nyingi sawa unachosema unaweza kupata kura mikoa yenye watu wengi tu Mwanza na Dar ukashinda ila sio ukubwa wa size maana Pwani na Morogoro wangekuwa wakubwa wakati Dar ndio mkoa mdogo sana Tz lakini population kubwa. Tungekuwa na mfumo kama wa USA ndio Dar na Mwanza zingekuwa muhimu kushinda ila kuna mikoa midogo ingekuwa na sauti kubwa kutuamulia kiongozi kama leo hii Nevada wenye 6 points wanawahukumu wenye 55 points.
 
Yeah, ni kweli imekuwa kitambo sasa hususan kwenye urais.

Lakini pia, si muda mrefu ulopita Arnold Schwarzenegger alikuwa two-term Governor wa California, 2003-2011. Yeye ni Republican. Na Governor ni statewide elected office.

George Pataki alikuwa Governor wa NY toka 1995 hadi 2006.

Yeye alitumikia mihula mitatu.

Kwa hiyo ni kweli, kwenye urais CA na NY mara ya mwisho kwenda GOP kwenye urais ilikuwa ni mwaka 1988 ambapo G.H.W. Bush alishinda landslide ya majimbo 44 au 46 dhidi ya Michael Dukakis.
 
Hii system ilikuwa ina maana zamani, karne za nyuma huko wakati uwiano wa watu kati ya jimbo moja na jingine ulikuwa mdogo. Chukulia Cali, yenye watu karibia mil 40 ije iamuliwe na Nevada yenye watu mil 3, hii ni sawa? Njia bora, kama ni lazima kuendelea na mfuno huu ni kuwa na split electoral votes kama walivyofanya Nebraska na Maine.
 
Kura zote za jimbo zikishahesabiwa, magavana huwa wanaweka sahihi ili ku certify electoral vote ya jimbo, hakuna gavana anayeweza kuharibu reputation yake kwa ku certify kura zenye utata.
 
Lakini kumbuka hizi ni states ni nchi zilizoungana kwa hiyo kama nchi zimeungana haijalishi size au wingi wa watu unahitaji kuwa na haki sawa. Tuchukulie mfano wa Tanzania ingekuwa kuwa ili uwe raisi wa muungano ni lazima upate 50% ya kura zote Zanzibar na 50 bara lakini kwa mfumo wetu Rais hata akipata zero kura Zanzibar atakuwa Raisi tu. Hata Zanzibar Unguja na Pemba ingekuwa lazima 50% hii inakupa uhalali vinginevyo mara nyingi pemba wanawakaa kijani lakini sababu wako wengi Unguja wanatawala tu ndio matatizo. kule wenzetu na udogo wako unapeleka Senators wawili kukuwakilisha kama nchi na kulinda haki ya katiba ya nchi, wanapokutana pale haijalishi wewe tajiri state yako au size nyinyi wote mko sawa sababu mmeungana.
 
Kutokana na hoja yako hiyo ya usawa kijimbo (kama nchi), kwa nini CA ina 55 electoral votes wakati ND ina 3?
 
Kutokana na hoja yako hiyo ya usawa kijimbo (kama nchi), kwa nini CA ina 55 electoral votes wakati ND ina 3?
Electoral votes walikubaliana iamuliwe na wingi wa watu sio utajiri sasa kwa mahesabu waliyopiga inamfanya mtu kuwa ngumu kushinda kwa kutegemea states zanye kura nyingi ndio mara nyingi hawa wadogo ndio wanakuwa wanaamua matokeo na kuonekana na wao wana sauti hawa waliondoka hii system akili kubwa maana wangekuwa wamefanya wingi wa kura tu mtu angekuwa anafanya kampeni CA, NY, Texas sijui NJ yaani sehemu yenye population tu huku sijui Nevada au N.H wasingekuwa na umuhimu, ila sasa Senators wanawakilisha state zao kwa usawa haijalishi wewe una watu Million 100 au Mil 3 wote wawili wawili kulinda haki za state katika usawa. System inaweza kuwa sio perfect 100% lakini inawa fit wao sana kutokana na history yao ya vita vya ndani.
 
Kuhusu mfano wa Zanzibar, niliwahi kumsikia Nyerere akisema kwamba, muungano wetu upo jinsi ulivyo [Zanzibar kuwa na serikali yake] ili kutokuwafanya Wazanzibari wasijisikie kumezwa na Tanzania bara kutokana na huo isiyo wao. Jambo ambalo yeye na wenzake waliliona ni la muhimu katika kuudumisha muungano.
 
Ndiyo maana nikasema majimbo yangerekebisha utaratibu ili kuwe na mfumo kama ule wa Maine na Nebraska. Na hii siyo mimi tuu nayeiona, wamarekani wengi sana wamekuwa wakijadili hili hivi karibuni, hasa pale Trump aliposhinda uchaguzi wa 2016, huku akiwa amepigiwa kura na watu wachache.
 
Wa Zanzibar wanaweza kujibu kama wanajisikiaje? ila ukiniuliza mimi nawaona kama mkoa tu madaraka yao yako limited ni majina tofauti tu lakini utendaji ni kama wa mikuu wa mkoa na wakurugenzi sio kama nchi majina tu tofauti ya position. Hakuna nchi moja ikawa na maraisi wawili ni jina tu hakuna lingine. kosa lao kubwa walilofanya sio muungano, muungano mzuri kwao kama ulivyokuwa kwetu kiusalama na kiuchumi tatizo walivyounganisha vyama hapo wakajitoa kafara. Na uhakika Zanzibar wasingeungana wangekuwa wanapinduana kila leo maana wamegawanyika sana hata wao ndani, sio unguja na Pemba tu hata ndani ya Unguja kuna matabaka kuna watu wanajiona wana mapinduzi na wana haki juu ya wengine, usalama wao ni kubaki ndani ya muungano tu. swali la system gani ya muungano hilo ni suala jingine sina jibu kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…