Biden amteua Mmarekani mwenye asili ya India kuongoza Benki ya Dunia

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
322
255
Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Alhamisi alimteua mtendaji mkuu wa zamani wa Mastercard Ajay Banga kuongoza Benki ya Dunia.

"Ajay ana uwezo wa kuongoza Benki ya Dunia katika wakati huu muhimu katika historia.

Ametumia zaidi ya miongo mitatu kujenga na kusimamia mafanikio ya makampuni ya kimataifa ambayo yanaunda nafasi za kazi na kuleta uwekezaji kwa zenye uchumi zinazoendelea kuimarika, na kuongoza mashirika kupitia vipindi vya mabadiliko.

Ana rekodi iliyothibitishwa ya kusimamia watu na mifumo, na kushirikiana na viongozi wa kimataifa kuleta matokeo," ilisoma taarifa ya Biden.

Banga, kiongozi wa biashara aliye na uzoefu mkubwa wa kuongoza mashirika yenye mafanikio katika nchi zinazoendelea, na uzoefu wa kuunda ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ili kushughulikia ushirikishwaji wa kifedha na mabadiliko ya hali ya hewa, atakuwa Rais wa Benki ya Dunia.

"Pia ana uzoefu mkubwa wa kuhamasisha rasilimali za umma na binafsi ili kukabiliana na changamoto za dharura za wakati wetu, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akiwa amelelewa nchini India, Ajay ana mtazamo wa kipekee kuhusu fursa na changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea na jinsi Benki ya Dunia inavyoweza kutekeleza ajenda yake kuu ya kupunguza umaskini na kupanua ustawi," ilisoma taarifa hiyo.

Uamuzi huo unakuja baada ya Rais wa Benki ya Dunia David Malpass kusema kwamba atajiuzulu karibu mwaka mmoja, mapema, kutoka kwenyeb wadhifa wake.

Kujiondoa kwa Malpass kumekuja miezi kadhaa baada ya wito wa kumtaka aachie ngazi baada ya kukataa kukiri makubaliano ya kisayansi kwamba nishati ya kisukuku inaongeza joto kwenye sayari.

Malpass alikabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa hali ya hewa mnamo Septemba baada ya kukataa kuthibitisha wakati wa jopo la hali ya hewa, ikiwa alikubali makubaliano ya kisayansi kwamba uchomaji wa nishati ya kisukuku ulikuwa unaongeza joto kwenye sayari, iliripoti CNN.

Kwa sasa Banga anahudumu kama Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya General Atlantic. Hapo awali, alikuwa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Mastercard, akiongoza kampuni hiyo kupitia mabadiliko ya kimkakati, kiteknolojia na kitamaduni.

Katika kipindi cha kazi zake, amekuwa kiongozi wa kimataifa katika sekta za teknolojia, data, huduma za kifedha, na ujumuishwaji.

Yeye ndiye Mwenyekiti wa Heshima wa Chama cha Kimataifa cha Biashara, akihudumu kama Mwenyekiti kuanzia 2020-2022.

Pia, ni Mwenyekiti wa Exor na Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Temasek.

Amekuwa mshauri wa mfuko wa General Atlantic unaozingatia hali ya hewa, BeyondNetZero, wakati wa kuanzishwa kwake mnamo 2021.

Hapo awali alihudumu katika Bodi za Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani, Kraft Foods, na Dow Inc.

Banga pia amefanya kazi kwa karibu na Makamu wa Rais Harris, kama Mwenyekiti Mwenza wa Ubia wa Amerika ya Kati.

Yeye ni mjumbe wa Trilateral Commission, mdhamini mwanzilishi wa Jukwaa la Ushirikiano wa Kimkakati la Marekani na India, mjumbe wa zamani wa Kamati ya Kitaifa ya Mahusiano ya Marekani na China, na Mwenyekiti wa American India Foundation.

Yeye ni mwanzilishi mwenza wa The Cyber Readiness Institute, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Kiuchumi ya New York, na aliwahi kuwa mjumbe wa Tume ya Rais Obama ya Kuimarisha Usalama wa Kitaifa wa Mtandao.

Yeye ni mjumbe wa zamani wa Kamati ya Ushauri ya Rais wa Marekani kwa Sera ya Biashara na Majadiliano.

Banga alitunukiwa nishani ya Foreign Policy Association Medal mnamo 2012, Padma Shri na Rais wa India mnamo 2016, Nishani ya Heshima ya Ellis Island, na Business Council for International Understanding's Global Leadership Award mnamo 2019, na Distinguished Friends of Singapore Public Service Star mnamo 2021.

Benki ya Dunia ambayo ni kundi la mataifa 187, inatoa mikopo kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia kupunguza umaskini.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alimteua Malpass kuwa mkuu wa Benki ya Dunia mnamo 2019, kwa kipindi cha miaka mitano. Kama mbia mkubwa zaidi, Marekani kwa kawaida huteua rais wake.
The_President%2C_Shri_Pranab_Mukherjee_presenting_the_Padma_Shri_Award_to_Shri_Ajaypal_Singh_B...jpg
 
Yaani Kuna India na China mmojawapo Ni future USA na USA atakuwa either India ama Sri Lanka.
What goes up must come down yaani must come down whether you like or not. Hawa jamaa ndio ma CEO wa kampuni kubwa USA na Europe.
Sie tunaleta kampeni ya kuzaa kwa mpango. Cheki Nigeria population inafanya anakuja juu kiuchumi.ushindani mhimu
 
Dunia ya kwanza wako makini sana katika vetting, huweziamini tangu huyo Jamaa azaliwe alikuwa akifatiliwa kila nyanya ya;

Thinking sharpness.

Best practices.

Disciplines.

Talent display.

Self attitude.

Job careers.

Decision making.

Personal trait.

Social relationship and participation.
 
Yaani Kuna India na China mmojawapo Ni future USA na USA atakuwa either India ama Sri Lanka.
What goes up must come down yaani must come down whether you like or not. Hawa jamaa ndio ma CEO wa kampuni kubwa USA na Europe.
Sie tunaleta kampeni ya kuzaa kwa mpango. Cheki Nigeria population inafanya anakuja juu kiuchumi.ushindani mhimu
Ona huyu nae. Matanzania mna reason kipuuzi sana ndiyo maana wengi mnashabikiaga upumbavu.
I'm sure we dingi una mke na watoto lakini reasoning ipo chini kabisa.
Naionea huruma Tanzania yangu.
 
Attachments

  • Screenshot_20230225-144716_Chrome.jpg
    Screenshot_20230225-144716_Chrome.jpg
    159.9 KB · Views: 2
Mawazo ya hovyo sana haya yako.

Back
Top Bottom