Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Kitabu kilichoandikwa na Nabii wa Mungu wa Ibrahim Isaac na Jakob hakiwezi kuwa cha kipagani..labda hilo kanisa lenye hayo maelezo liwe haya madhehebu ya wachawi na wachumia tumbo wa miaka hii ya karibuni.
Basi tusaidie kwanini kitabu cha Nabii Gadi hakipo kwenye biblia??? Kwanini kitabu cha Jasher na Enoko havipo katika Biblia??
 
Dini inaingiaje hapa?? Tujikite kwenye hoja kwamba JF wafia dini mbadilike mfungue akili yenu na mkubali maarifa kutoka vyanzo tofauti sio kila hoja mpaka bible

Anyway nimeweka hapo maswali labda tusaidiane kujadili hayo tupate majibu
Nimehoji dini yako maana katika maandiko yako nimeona alama zenye harufu isio nzuri. Pia kukusaidia kila dini na ibada yake kuna uhusika wa roho au viumbe vyenye nguvu visivyoonekana.kila dini kuna roho yenye kuambatana nayo, ukristo una roho yenye kuambatana nao, hivyo kama kuna cha kuhoji au kisichoeleweka ataulizwa huyo roho na atatoa majibu yalio kamili. Sio watu kutafuta Maarifa kwenye vitabu vilivyoandikwa kwa akili nyepesi isiyo na mashiko.
 
Nimekuelewa mkuu sasa basi kwa maoni yako vitabu hivyo wote tunafahamu kuwa vinaitwa Pseudepigraphi yaani havitambuliki na kanisa je ni kwanini Biblia inavitolea reference??? Na kama Biblia inavitolea reference je ni kwanini bado havitambuliki na kanisa mpaka leo?? Na je tukijengea hoja kupitia hivyo vitabu tunakuwa sahihi??

Nina shauku sana ya kuelewa hii sintofahamu, ubarikiwe
 
Mtazamo wangu,

Kwa ujumla, dini(imani) ambazo hua zinatumia maandiko/vitabu yalioshushwa/vilivyoshushwa toka mbinguni (Mfano hizi mbili, Christianity - Bible, Islam -Quran) kwenye swala la reference kuhusiana na mambo/jambo ambalo halipo katika hayo maandiko/vitabu (1st Reference), hua wanaruhusiwa na baadhi ya articles kurefer katika vitabu vingine.

Kwa kifupi, hakuna kitabu/maandiko yoyote ambayo yapo STRICTLY FIXED WITHOUT OTHER REFERENCE, vitabu vyote vina exeption clause ya reference (for further reference).

Mfano mmoja mzuri ametoa zitto junior kuhusiana na thread yake ya bible, ambao namuunga mkono kwa alichoandika 100%.

Mfano wa pili, hata waislamu pindi wanapokutana na jambo ambalo halipo/halijawekwa wazi katika Quran, hua wana refer kwenye vitabu vingine (Kama vile vitabu vya Hadith - Vitabu vya Bukhari Na Muslim n.k).


Kwa mwenye idea ya maswala/elimu ya Theology natumai atakua amenielewa.
 
Basi tusaidie kwanini kitabu cha Nabii Gadi hakipo kwenye biblia??? Kwanini kitabu cha Jasher na Enoko havipo katika Biblia??
Wakijibu hili swali na mimi nachangia kwa hoja na ufanisi mkubwa ili jamii itambue umuhimu wa kuficha vitabu kadhaaa katika biblia na kuifanya jamii kushindwa kuconnect dots ili kupata mtiririko mzuri wa jinsi ulimwengu wa mwanadamu ulivyopata kuwa..


Pia kuna vitabu kama the Gospel of Mary Magdalena havipo kwenye biblia ya leo..

The Gospal of Thomas pia inakosekana katika edition mpya kitu ambacho ukimtolea reference mtu aliyebase na edition ya sasa hivi mtabishana mpaka kunakucha..

The Gospal of the lost twins kinakosekana kwenye edition ya bible iliyopo...

Yan wakati hivyo vitabu ndo vinajaribu kuwa na source at least ya kuweza kupata walau moja mbili tatu juu ya ukweli wote..

The last Super inaelezewa vizuri tena kwa mfumo mkubwa sana wa itifaki lakini kinakosa nafasi ya kuingizwa kwenye biblia iliyopo..

Mpaka hapo nachoka kwa uchovu mkubwa sana juu ya bibl kuwa kama source pekee ya kila kitu kinachohujiwa ndani...


The bible can not be the source of informations and at the same time stands as a reference point to explain the inside mentioned issues.
 
Twende taratibu..... Biblia yenyewe ndio inatoa reference alafu unataka tusijengee hoja kupitia hivyo vitabu mpaka tukaombe kwanza?? Anyway ningependa unipe jibu straight bila kuzunguka zunguka

Je kwanini vitabu hivyo viliachwa ilihali biblia imevirefer??

Na kama Biblia imevirefer ni kwanini tukijengea hoja mnazipinga kisa tu zipo nje ya Biblia??

Embu naomba ujibu hayo usikimbilie kumuingiza Roho mtakatifu ilihali ulipoanza ulitumia akili zako binafsi alafu sasa ndio unamrushia kesi.....

Nasubiri
 
Basi tusaidie kwanini kitabu cha Nabii Gadi hakipo kwenye biblia??? Kwanini kitabu cha Jasher na Enoko havipo katika Biblia??
Kitabu cha Gadi kinahusu matukio yaliohusiana na utawala wa daudi maana gadi alikuwa nabii wa daudi kumwelewesha yale Mungu aliyotaka ayafanye,,kitabu cha yashari kimeandikwa Wakati wa utawala wa Suleiman na baadhi waliomrithi ufalme,,,wamekiita kitabu cha tarehe,,,yaani rekodi ya matukio,,,kwa leo tungekuwa tunaita diary....

Inawezekana kulikuwa na mambo ya kuandikwa na yaliandikwa kwa sehemu na ndio maana umevijua ila biblia zote sahihi ni maandiko yaliochaguliwa kwa mwongozo wa roho alie nyuma ya ukristo ili kuwaelewesha Mambo ya adili wakristo na sio wasome diary zenye history ya wafalme pasi na kuwa hizo Habari zina elimu kwa maisha ya kiroho ya wakristo.
 
lifecoded,
Dah mkuu umenigusa sana..... Umeshasoma gospel of judas iskariot?? Imenifungua kichwa sana itabidi nianzishie uzi wake kabisa maana inaelezea chanzo halisi cha Yuda kumsaliti Yesu na "injili" ya kweli ambayo Yuda pekee ndio alipewa na mengine mengi yenye uhalisia ila ndio hivyo kimetolewa nacho..... Anyway nasubiri mkuu utueleze kidogo hapo kuhusiana na sababu kwanini baadhi ya vitabu imebidi vifichwe

Ubarikiwe
 

Wewe unacho hicho kidayari/ki diary?? Ni hoja ipi uliijenga kupitia hivyo vitabu ikakataliwa,,,je unajua unakosea kuviita vya kipagani??au unataka hata ukijenga hoja kwa vitabu visivyo na muunganiko na ukristo ukubaliwe tu usipingwe??? Hayo ni mambo yanayowezekana kwenye physics math na bios,,sio dini ya ukristo
 
Mtoa mada, Naomba kukuuliza...
Je unaamini katika Biblia? na kwamba Mungu anaongea na sisi kupitia hiyo?
Kama hauamini basi ni halali yako kuhoji kwa namna hiyo.

NB; nimeuliza hayo kutokana na mada zako nyingi zinazohusu dini, Nadhani vitu vingine tutamuuliza Mungu tukifanikiwa kufika huko.
 
Kwa usahihi tamko tarehe limetoholewa kutoka katika lugha ya kiarabu likitamkwa "Tarekh". Kwa maana ya tamko hilo kilugha ni Historia.

Ukiambiwa rejea tarehe ya fulani,aidha ni kitabu cha muandishi fulani kinaelezea historia fulani au historia ya mtu fulani. Huo ndio usahihi wa maana ya tamko "Tarehe".

Naendelea kusoma kupata faida......
 
1.Sasa kama hivyo vitabu ndio Biblia inasema vina historia kamili ya Daudi kwanini tukijengea hoja mnakataa?? Gadi kaongelea mengi ya Daudi ambayo Biblia haiyasemi je kwanini mnapinga hoja zake??

2.Na kama hivyo vitabu ni halali kwanini kwenye biblia haviwekwi??

3.Unaposema Vitabu vilivyowekwa kwa sasa vinasaidia wakristo hivyo vya Gadi havina maana je nkikuuliza kitabu cha wimbo ulio Bora unasaidiaje ukristo wako?? Au kitabu cha Samuel kina tofauti gani na kitabu cha Gadi kiasi mkiache ilihali vinafanana content??

Naomba ujibu kwa mtiririko huu huu
 
Nashukuru mkuu kwa clarification yako
 
Kwa kukusaidia vilivyoandikwa kwenye Bible ni vile tu vilivyokuwa tested na kuthibitika kweli, yale yasiyo na uhakika japo yaweza kuwa kweli yakatupwa nje.
Mkuu labda sijaeleweka
1. Biblia inatoa reference kuwa story nzima ya Daudi au rehoboam etc zinapatikana kwenye vitabu A, B na C??

Sasa swali linakuja kwanini tukifanyia reference vitabu hivyo hasa humu JF mada inapingwa kisa tu haipo kwenye Biblia??

Yaani why Biblia imefanyia reference ila sisi tukifanyia reference haikubaliki kwa mada za kiimani??
 
Tuko pamoja bro,kuna mifano kadhaa ya vitabu fulani nilitaka kuiweka hapa ila nikaona haina haja sana.

Tuendelee......
Karibu mkuu umwage nondo kwa faida ya wanajukwaa wote
 
Yes mkuu namuamini Mungu sana tu na ninaamini katika Biblia sana tu ila huwa napenda kuhoji mambo ambayo nayaona yanasintofahamu kwa lengo la kujifunza zaidi so hakuna kosa lolote hapo.

Na nafikiri kuhoji ni vizuri ili upanuke uelewa ndio maana Hata shuleni mwalimu akifundisha tunamhoji maswali naye anatupa majibu. Na nikiri tu kuna watu huwa kupitia mijadala ndio wanasoma Biblia ila bila kuwepo maswali hawawezi soma Biblia kwa undani zaidi.

Na nitoe changamoto tu kwa wakristo na waislam kuwa tujenge mazoea ya kupenda mijadala sababu mtakutana na asiyeamini utakosa hoja za kumhubiria

Ni hayo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…