Biblia, Korani zinapotumika vibaya

Biblia, Korani zinapotumika vibaya

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,208
Biblia na Korani ni vitabu vitakatifu lakini wakati mwingine ni chanzo cha chuki, mifarakano na machafuko duniani kote.

Mmesikia yaliyotokea Pakistan wiki hii ambapo kuachiwa huru kwa Asia Bibi kumeacha machafuko mitaani.

Watu wanaitaka roho ya dada huyo mkristu aliyejikuta matatani katika nchi hiyo ya kiislamu baada ya kutokea kaubishi na wanawake wenzake wa kiislamu. Alidaiwa "kumkufuru" Mtume Mohamed.

Wanawake wale wa kiislamu ndio walikuwa wa kwanza kum provoke Asia baada ya kukataa kutumia chombo alichotumia kunywa maji, kwa vile yeye si Muislamu.

Ubishi kidogo tu watu wanataka kuitoa roho ya mtu! Watu hao wauaji nao wanajiita Waislamu dini ya Allah.

Tujiulize watu hao wanaoua wenzao kwa kisingizio cha dini wao ni wasafi kiasi gani.... ( Usihukumu! Utahukumiwa!)

Ukweli ni kwamba vitabu hivi ni mwongozo wa dini. Hata hivyo wakati mwingine vimekuwa chanzo cha mateso na fujo duniani.

Wako watu wanajifanya watetezi wa dini lakini deep inside wanaitumia Koran kwa malengo ya kisiasa na au kukomoana.

Baadhi ya ndugu zetu wachungaji wanaitumia Biblia kama njia ya kujipatia utajiri. Ndio maana Tanzania ina utitiri wa makanisa. Huko Afrika Kusini kuna makanisa mpaka ya wanawake watupu!

Ukweli ni kwamba vitabu hivi ni pasua kichwa kweli kweli na kila anayeanzisha kanisa anakuja na tafsiri yake na kila kiongozi wa msikiti ana uelewa wake juu ya Koran.

Kwa ujumla dini hazikumbatii homosexuals lakini kuna baadhi ya makanisa yanayotumia Biblia hiyohiyo wanapokea gays and lesbians! Kuna makanisa yana hadi maaskofu ......ga!

Ujumbe ulioko kwenye vitabu hivi vya dini ni muhimu ingawa sidhani kama aya zooooote zinaendana na dunia ya sasa. Let's be practical.
Watu wanatenda maovu lakini nadhani ni dhambi kubwa zaidi kuitumia Koran au Biblia kuwadhulumu watu.

Tujipange vyema yanayotokea Pakistan yasije kamwe kutokea Tanzania. 'Religious tolerance' ni muhimu sana kwani dunia ya sasa ina mchanganyiko wa watu mbalimbali kila kona.
 
Tafadhali..
Qur'an sio takatifu ni Tukufu, Biblia pekee ndio takatifu. Unaweza kua mtukufu ila usiwe mtakatifu. Mtukufu Mfalme Magufuli hawezi kua mtakatifu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom