Bibi wa miaka 79 awa mfano wa mabadiliko, ni mwanachadema hasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi wa miaka 79 awa mfano wa mabadiliko, ni mwanachadema hasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikivembu, Jul 3, 2012.

 1. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Nilikutana na bibi mmoja leo akiwa anapita kwenye mitaa ya mjini akiwa na begi lake begani, shingoni kafunga skafu ya chadema na amening’iniza kitambulisho cha aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dr Wilibrod Slaa.Nikavutiwa sana.Ilinibidi nianze kumfuatilia kwa lengo la kutaka kumhoji kulikoni bibi kizee kama yeye amevalia nembo za chama pinzani.Nikamsalimia na kuanza kuhojiana naye.Wakati huo nilikuwa nimeficha kamera yangu kwa hofu kuwa huenda angekataa kupigwa picha.
  Mahojiano
  Ngalikivembu:Bibi imekuwaje umevalia skafu na kitambulisho hiki wakati wewe ni mzee?
  Bibi Agness: Mimi ni mmoja wa wanachama wa chadema.Nataka mabadiliko.
  Ngalikivembu: Lakini wazee kama nyie si ndo mmeshikilia ccm?
  Bibi Agness: Hapana.Mimi nahitaji mabadiliko sana.Hawa kina kikwete wanatutesa.
  Ngalikivembu: Viongozi wa chadema wanakujua?
  Bibi Agness: Wananifahamu sana.Na pia viongozi hao wakija hapa lazima tuonane.
  Ngalikivembu; Viongozi gain wewe unawajua?
  Bibi Agness: Halima Mdee, yule aliyefariki, alikuwa anaitwa Regia Mtema.Mwaka jana alikuja hapa tarehe 7 Desemba na 17 Desemba.(katika umri wake huo bado anakumbukumbu sana).
  Ngalikivembu: Unaishi wapi hapa mjini?
  Bibi Agness: Lizaboni.
  Ngalikivembu: Kule mliko fanya mabadiliko ya diwani mwezi wa nne?
  Bibi Agness: Ndio.Na anafanya kazi sana.Anapendwa mno.Mimi nilipita kufanya kampeni sana.
  Ngalikivembu: Kiumri nakuona kama umetimiza miaka 80?
  Bibi Agness: Hapana nina miaka 79.Mwakani natimiza hiyo miaka.
  Ngalikivembu:Hongera sana bibi.
  Bibi Agness: Asante sana.
  Ngalikivembu: Unaitwa nani?
  Bibi Agness: Naitwa Agness Zomari
  Ngalikivembu: Naomba nikupige picha
  Bibi Agness: Haya. Piga tu.Subiri niweke sawa kofia yangu.
  Mwisho tukaagana
  Ngalikivembu: Asante bibi kwa heri
  Bibi Agness:Mungu akubariki.
   

  Attached Files:

 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Njaa haina mwenyewe hata hii njaa ya mabadiliko haina mwenyewe, mpe bi hongera zake na ungemwambia aendelee na ukombozi la taifa letu.
   
 3. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu hongera maana mbali na kumuona, ulijitahidi kufanya nae mahojiano na kumalizia na ka-picha.Safi sana.Nina imani kufikia 2015 watu wengi sana watakuwa wamepata mwanga kisiasa,polepole tutafika.
   
 4. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  mbona mtaani watoto kibao wana masingle yao ya CDM(variant ya ile anthem ya peoples power)
   
Loading...