kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
Mwanamke mmoja wa nchini Romania amekuwa bibi mwenye umri mdogo kuliko wote duniani baada ya mtoto wake wa kike aliyemzaa alipokuwa na umri wa miaka 12 naye amefanikiwa kujifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 11.
Rifca Stanescu alipopata ujauzito akiwa na umri wa miaka 12, hakutaka mtoto wake huyo afuate nyayo zake na kuangukia kwenye mimba akiwa na umri mdogo.
Lakini binti yake huyo akiwa na umri wa miaka 11 tu amefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume ambaye amempa jina la Ion.
Rifca ambaye sasa ana umri wa miaka 23, amekuwa bibi mwenye umri mdogo kuliko wanawake wote duniani.
Taarifa zimesema kuwa Rifca akiwa na umri wa miaka 11, akihofia wazazi wake wangemuozesha kwa mwanaume mmoja kijijini kwao, alitoroka nyumbani kwao na kwenda kuolewa na mpenzi wake Ionel ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 13.
Miezi michache baadae Rifca alipata ujauzito na alifungua mtoto wake alipokuwa na umri wa miaka 12.
Rifca alimpa jina la Maria mtoto huyo , alidhamiria kumpa malezi bora mtoto wake ili asije kuangukia kufuata nyayo zake.
Lakini Maria alipokuwa na umri wa miaka 10, aliacha shule na kwenda kuolewa mtoto mwenzie na miezi sita baadae alipata ujauzito.
Maria alijifungua mtoto wa kiume ambaye alimpa jina la Ion. Rifca amekuwa bibi akiwa na umri wa miaka 23 wakati mama yake Rifca amefanikiwa kumuona kituu wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 40.
"Nimefurahi kuwa bibi mdogo kuliko wanawake wote duniani, lakini sikupenda Maria kupata ujauzito akiwa na umri mdogo kama huu", alisema Rifca huku akimkumbatia mjukuu wake.