Bibi Harusi wa zamani na wa sasa

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
2,674
2,801
ZAMANI KIDOGO MIAKA YA 1999 kurudi nyuma MABIBI HARUSI walikuwa wakilia kwenye harus MATRON walikua na kazi za kuwafuta machozi adi leso tatu au nne...SASA HIVI MABIBI HARUSU, wanaimba, wanacheka wanacheza kwaito had viduku....NAHOJI TU, ...Kilichokua kinawaliza wazaman nini, na kinachowafurahsha wasiku izi ni nin?....kila mtu aniambie wazo lake.
 
Wa zamani walikuwa wanalizwa maana ndoa zilikuwa na vipigo sana.

Kwa sababu ya kupungua kwa vipigo ndani ya ndoa wa siku hizi wanacheza maana wanajua huko wanakokwenda ni mwendo wa kubebishwa tu.

Yaani mambo mteremkoooooo.
 
Hawa wa sasa anaingia katika ndoa wakiwa na uzoefu wa kutosha na washalizoea dushelele ila wale wazamani walikuwa wageni wa kila kitu

Hawa mtu anaolewa kashakaa kinyumba na bwana miaka sita pika pakuwa unategema atalia nini sasa zaidi ya kufurahi
 
Ushasema zaman na sasaivi..... Tayari ni maneno mawili tofauti. Mambo hayawezi kuwa yaleyale
 
Zamani siku ya harusi ndo siku unatoka kwenu na ndo siku unaanza kukaa mbali na nyumban tofaut na watu wengi sikuhiz alaf pia utandawazi kulia ni ushamba sasa unalia nin coz ndoa ni jambo la furaha labda ulie machoz ya furaha tu kidogo
 
Tena walikuwa muda wote wanaangalia chini kama kwa aibu fulani hivi

Ila siku hizi bibi harusi anaangaza ukumbi mzima kucheki orodha ya mabest zake waliohudhuria
 
ZAMANI KIDOGO MIAKA YA 1999 kurudi nyuma MABIBI HARUSI walikuwa wakilia kwenye harus MATRON walikua na kazi za kuwafuta machozi adi leso tatu au nne...SASA HIVI MABIBI HARUSU, wanaimba, wanacheka wanacheza kwaito had viduku....NAHOJI TU, ...Kilichokua kinawaliza wazaman nini, na kinachowafurahsha wasiku izi ni nin?....kila mtu aniambie wazo lake.
Walikuwa wakihofia maisha mapya ya kuishi na Me lakin hawa wa sasa unakuta mpaka anaolewa ashatembea nayo huyo bwana Mara nyingi kwaiyo hata siku ya harusi haoni jipya zaidi ya kufurahi kuingia kwenye list ya waliyo olewa
 
Zamani wengi walikuwa wanaolewa na wanaume wasiowajua vizuri coz wengi walikuwa wanachaguliwa wachumba.but siku hizi wachumba huchaguana na kujipa nafasi ya kufahamiana kwa muda mrefu kiasi ambacho hata ndoa wanakuwa wanaililia na kulazimisha ifungwe mapema.Hivyo siku ya harusi ikifika lazima wacheze sana kwaito.
 
Kwanza rujue wewe ni wa zamani au wa sasa?
Kama wa zamani je ulilia?

Kama wa sasa ulicheza taarabu?
 
Back
Top Bottom