Bibi aweka kizuizi barabarani na kutoza magari, pikipiki ushuru

Ground Zero

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
342
95
IMG_20110526_113912.jpg IMG_20110526_113529.jpg IMG_20110526_113540.jpg Bibi ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa madai kwamba sharti apewe chochote amekutwa akiwa ameweka kizuizi kwenye barabara inayopita mbele ya nyumba yake eneo la Mabibo Hostel, Ubungo jijijini Dar na kutoza kiasi cha shilingi 500 kwa waendesha pikipiki na magari. Alipoulizwa ni kwa nini ameweka kizuizi alidai kuwa anakusanya fedha kutoka kwa wenye magari na pikipiki ili aweze kuweka kifusi cha mchanga.

Je serikali inajua hilo?kila mtu akiweka barrier na kutoza kodi nchi itatawalika?Itakumbukwa wiki iliyopita Mh Spika naye aliamua kufunga barabara kule sinza japo yeye hakutoza ushuru.

Nawasilisha
GZ
 
Jamani Tz kuna vituko. Huenda hali ya maisha ni ngumu jamani. Sasa akale wapi. Kila kitu bei imepandishwa. Halafu cha ajabu hao hao ndo wanakuwa wa kwanza kuchagua chama cha magamba
 
Tanzania hii, kama na ww unataka kaweke Tazara pale kusanya mia mia mpaka waje wastuke umepata za kutosha, hujasikia Daktari wa ngara?
 
LOL. Nimecheka kweli. Nadhani anaiga mfano kutoka kwa viongozi. Niliona humu jamvini kuwa speaker wa bunge alifunga naye barabara kabisa! Kuna siku moja nilikuwa naendesha gari mjini Dar na njia yenyewe ilikuwa 'oneway'. Mara gari likatokea upande wa pili. Nilisimama ghafla na kumpisha mbabe yule. Kuniona nimeshtuka sana aliniambia, "Unashangaa nini kaka, nchi hii hakuna sheria"! Bongo mwendo mdundo.
 
Huyo Bibi sio kama anatoza ushuru bali hali ya maisha imezidi kuwa ngumu chini ya serikali ya ccm. hiyo ni njia mojawapo ya kuomba ndio ina maana serikali iliyopo madarakani iondoke.
 
Huyo Bibi sio kama anatoza ushuru bali hali ya maisha imezidi kuwa ngumu chini ya serikali ya ccm. hiyo ni njia mojawapo ya kuomba ndio ina maana serikali iliyopo madarakani iondoke.

serikali iwape watu hela? kutoka kwenye kodi za wazungu na wajapani waliopigwa tsunami?
 
sasa mnataka naye akale wapi? TRA wezi, viongozi serikalini wezi tena wa mabilioni yeye jero tu! mwacheni, kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake, kilichobaki tugawane nchi kila mtu atoze kodi sehemu yake!
 
Back
Top Bottom