Biashara za wadaiwa wa kodi bado zinafungwa kinyemela

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Awamu ya sita baada ya kuingia madaraka iliagiza TRA kuacha kufunga biashara za wafanyabiashara ambao wanadaiwa kodi na badala yake watumie njia laini katika ukusanyaji kodi.

Kinyume chake taasisi za utoaji wa leseni kama halmashauri na Brela zinafunga biashara kimbinu kwa kuomba kitu kinaitwa TAX CLEARANCE ili kutoa leseni.

Hii inamaanisha kuwa bila tax clearance hupati leseni na bila leseni huwezi kufanya biashara,hii ni sawa au haina tofauti na kuwekewa kufuli na TRA.

Nashauri serikali kutofautisha majukumu ya mamlaka za leseni na TRA ili TRA isitumie vibaya mamlaka za leseni kama njia ya kumlazimisha mfanyabiashara kulipa kodi hata kama haridhiki na kiwango alichopangiwa aweze kuendelea na biashara wakati wanaendelea kujadiliana na TRA
 
Back
Top Bottom