Biashara za udalali ni jipu la kutumbuliwa

MAFUNGUO KUFULI

Senior Member
Jul 28, 2015
138
39
Serikali Haina Budi Kubana Biashara zote za Udalali;

=Udalali Wa Nyumba Za Kupanga,
=Udalali Wa Mazao Ya Mashamba,
=Udalali Wa Madini;
Nk.

Hapa Mamilioni Ya Kodi Yanapotea Kwa Uholela Wa Madalali Hawa Ucharwa.
 
Umesahau

Udalali wa ardhi
Udalali wa magari
Udalali wa simu
Udalali wa wasanii

Yani kila sehemu na wananikera hawa watu,najinafikisha kua rafiki yao.
 
Hata kupata nafasi ya mwanao darasa la kwanza shule kama Diamond au Olympio bila dalali hupati
 
madalali noma....unaulizia chumba anakwambia kipo mtaa wa 2 ila kukupeleka tu elf 5.... haijalishi chumba utakichukua au laa......
 
Hawa watu watafute chakufanya, haiwezekani mwanaume mzima unaishi kwa ujanja ujanja na kubahatisha. Nendeni mkalime
 
Wameshakupiga kwenye ela ya pango?ila wanafaida pia usifikirie upande mmoja .serikali iweke mazingira tu wote wapate vibali na wao walipe kodi.udalali upo kote duniani
Situmiagi dalali mimi,natembea door to door mpaka kieleweke
 
Mwizi ni anaechukua kitu au pesa kwa nguvu au kwa kificho bila ya ruksa ya mwenyenacho, dalali unampa mwenyewe.
Madalali ni msaada unapohitaji kitu hujui kilipo na hujui utakipataje kinachokufaa na kwa wakati, kuna ambao sio waaminifu na njaa kali ndio huaribu kazi hii.
 
Hawa watu watafute chakufanya, haiwezekani mwanaume mzima unaishi kwa ujanja ujanja na kubahatisha. Nendeni mkalime
Heshimu kazi za watu. Mfano unatafuta nyumba,gari ya kununua unaweza wewe kuzunguka mji mzima kutafuta? Unaona rahisi sana mtu akija kukwambia nyumba au gari ikko sehemu fulani twende ukaone?
Kuna madalali wabaya kama ilivyo kuna wafanyakazi wa taaluma nyingine wabaya.
 
Madalali wote wasajiliwe na wawe wanalipa
kodi na pesa yake itolewe kutoka kwenye hizohizo za miez ya chumba co badala ya miez 6 atoe ya miez 7 mwezi 1 wa dalali huo ni unyonyaji.
 
Dalali huwa anarahishisha mambo atanila pesa ila na mimi nitakuwa naingiza pesa kwa kuwa muda wote nitakuwa kwenye kazi yeye anahangaika mwenyewe huko akipata nampa chake na mimi nabaki na changu
 
Back
Top Bottom