Biashara ya vyuma chakavu yasitishwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279

Serikali imezuia biashara ya kuingiza na kusafirisha nje ya nchi taka zenye madhara vikiwamo vyuma chakavu, betri zilizotumika na taka za eletroniki mpaka utaratibu mpya utakapotolewa.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam jana, imewataka watu wanaojihusisha na biashara ya ukusanyaji, usafirishaji, urejerezaji wa vyuma chakavu, taka za elektroniki, taka za kemikali, mafuta machafu, taka zitokanazo na huduma za afya na betri zilizotumika kujiandikisha upya Baraza ka Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na kupata vibali vipya kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Utaratibu huo mpya utajumuisha ukaguzi wa uwezo wa waombaji wa kufanya shughuli hizo huku wafanyabishara wakionywa kutopokea taka hizo kutoka kwa mtu asiyekuwa na kibali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya ziara ya ghafla ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, katika Bandari ya Dar es Salaam.

Makamba alitoa maelekezo na maagizo kuhusu utaratibu mpya wa biashara ya taka zenye madhara, baada ya kuwapo ukiukwaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004, kanuni za sheria hiyo na Mkataba wa Kimataifa wa Basel kuhusu taka zenye madhara.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais inakusudia kubadilisha Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Mwaka 2009 na kuandika kanuni mpya za taka za elekroniki kuweka udhibiti bora zaidi.

Wakati serikali ikitoa agizo hilo, tayari kuna makontena 44 ya vyuma chakavu katika Bandari ya Dar es Salaam na Waziri Makamba na ujumbe wake wamekuta makontena 10.

“Lazima jambo hili lifuatiliwe kujua nani waliohusika na jambo hili wakati taarifa ya kusimamisha usafirishaji imekwisha kutolewa,” alisema.

Ilibainika kuwapo mzigo wa vyuma chakavu ulioingizwa nchini kwa majahazi kama “loose cargo” kutoka Comoro kupitia Zanzibar.

“Tunawasihi wananchi wote pia kutoa taarifa haraka kwa mamlaka husika, ikiwamo NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais, wanapohisi au kuona mtu au kampuni yoyote inaingiza nchini taka za aina yoyote kutoka nje ya nchi au ukusanyaji wa vyuma chakavu, taka za elektroniki na betri zilizotumika na utupaji wa taka za hospitali unafanyika kinyume cha utaratibu,” alisema Makamba katika taarifa hiyo.

Katika ziara hiyo, Waziri Makamba aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk. Samuel Gwamaka na maofisa waandamizi wa baraza hilo.
 
Kila biashara mnaharibu, badala ya kutengeneza mazingira mazur ya watu kujitafutia kipato mnazid kuwabana, mlianza kwenye mahind mkaja kahawa na korosho, kwote huko mmefail vibaya. Na huku mnakuja haribu tena.
 
Aisee hili ni pigo. Kuna watu wengi sana wanategemea hii biashara sijui itakuaje? Naona watapewa masharti magumu ambayo sio wengi watayaweza
 
Kila biashara mnaharibu, badala ya kutengeneza mazingira mazur ya watu kujitafutia kipato mnazid kuwabana, mlianza kwenye mahind mkaja kahawa na korosho, kwote huko mmefail vibaya. Na huku mnakuja haribu tena.
Ni ujinga wa hali ya juu sana. Hapo wamelenga wafanyabiashara wapigwe pesa ndefu. Biashara ilikuwepo miaka yote na haya hayakuwepo. Wamelenga soko lishuke na wanufaike kimtindo sababu watakuwa na viwanda vyao hivyo kujipatia kwa bei ya kutupa. Wachache sana hajaelewa ujanja uluofichwa kwenye tamko hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ujinga wa hali ya juu sana. Hapo wamelenga wafanyabiashara wapigwe pesa ndefu. Biashara ilikuwepo miaka yote na haya hayakuwepo. Wamelenga soko lishuke na wanufaike kimtindo sababu watakuwa na viwanda vyao hivyo kujipatia kwa bei ya kutupa. Wachache sana hajaelewa ujanja uluofichwa kwenye tamko hili

Sent using Jamii Forums mobile app
We acha tu yaan tumeingia sijui choo cha wapi. Yaan kila biashara wanataka wafanye wao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom