Biashara ya viazi soko la mabibo Dar es salaam

Biashara ya viazi soko la mabibo Dar es salaam

Hii inawezekana kwa mazao ya mahindi na mchele tu.
Kwenye viazi haiwezekani kwa sababu viazi ni bidhaa ya kuuza chap chap vikikaa sana vinaoza.

Kwa hiyo ni biashara ya kuuza ndani ya siku 3 mpaka siku 7 uwe umeshamaliza mzigo ukizidisha hapo vinakuozea unakula hasara.
Akitokea mtu smart hii fursa inawezekana. Akinunua kwa cash ananunua kwa bei punguzo maana wakulima hawatotaka risk ya kumwachia dalali wa kulipa baadae. Anachofanya huyu mnunuzi smart ni kuwa na hifadhi. Anakuwa dalali na msambazaji, ni kama retailer au market maker. Sema huo mtaji wake ni mrefu.
 
Bei ya gunia sasa ni 28000-33,000 kwa mbeya shambani (ntokela, ndaga) alaf kwa hyo pesa ni ndogo sana kuchukua mzigo kutoka mbeya mpaka dar labda ingefika ata 5M ndo ukaanza hyo labda izungushie dsm tu kwenye masoko madogo.
 
Natafuta mtu anayefanya biashara za namna hii,
Yaani anachukua bidhaa kwenye masoko makubwa na kupeleka kwenye masoko madogo Kama yupo humu tuwasikiane niweze kujifunza kupitia kwake
 
Akitokea mtu smart hii fursa inawezekana. Akinunua kwa cash ananunua kwa bei punguzo maana wakulima hawatotaka risk ya kumwachia dalali wa kulipa baadae. Anachofanya huyu mnunuzi smart ni kuwa na hifadhi. Anakuwa dalali na msambazaji, ni kama retailer au market maker. Sema huo mtaji wake ni mrefu.
Mkuu viazi ni Mali ya kuoza. Siyo kwamba watu hawawezi weka Pesa yao, Ila wanaikwepa risk ya mzigo kugoma kutoka afu unakuozea..

Kwa hiyo wanasubirisha malipo ili in case mzigo usipotoka au ukibaki mchache wanamkabidhi Mkulima mzigo wake wanahamia kwa Mkulima mwingine mwenye mzigo fresh.

Afu ujinga Wa hizi Mali, ni kwamba mzigo ukilala, kesho yake ukaingia mzigo mwingine, wewe uliyelaza lazima ushushe bei maana wanunuzi hukimbilia mzigo Mpya ambao ni fresh zaidi.
 
Sela Son, Tengeneza connection kwanza na madalali wa hapo sokoni kabla hujaenda kununua mzigo shambani, tofauti na hapo upo kwenye risk ya kupata hasara...Goodluck
 
  • Thanks
Reactions: amu
Njombe to dar Gali ni 1.3milion

Baki huko huko ununue na kuuza huko huko

Japo kuwa kama una hakika na Soko kwenye gari una Lipa baada ya kufika sokon kwaiyo unaweza ukanza
 
Mambo vipi wanajamvi! MTU wenu Leo Niko hapa kuulizia kuhusu biashara ya viazi kutoka huko vitokapo ( iringa,mbeya) mpaka kuingia sokoni Mabibo Dar es salaam. Kwa kuanza.
1_bei ya gunia moja shambani.
2-gharama za usafirishaji.
3-je nahitajika kuwa na leseni?
4-mbinu za ujanja ujanja sokoni
5-bei ya gunia sokoni.
Mwisho kabisa Nina TSH 1.2 milioni nataka kuanza biashara hii , either nikiwa Kama dalali au mfanyabiashara mpokezi kutoka kwa madalali na kuuza hapahapa sokoni!
Hili nimelileta ili kusaidiwa c hapa ndani uwanjani hakifeli kitu.
Nawasilisha.
MTU wenu Sela son
Njoo pm mkuu ninamtu mkulima wa viat vizur na saiz anakaribia kuvuna njoo nikuconect naye
 
Nimefanya kilimo cha viazi lakini kwa soko lilivo Bora niviuzie shambani hukohuko.
 
Nimefanya kilimo cha viazi lakini kwa soko lilivo Bora niviuzie shambani hukohuko,
Mkulima ni bora ukauzia shambani kama kuna uwezekano ila kuja sokoni labda uuze kwa direct customers lakini kwa dalali ni stress tu.
 
Nimewahi kufanya biashara hii 2018 nikajakuacha baada ya kula hasara kubwa.

1. Tengeneza mahusiano mazuri na dalali ambaye unataka kufanya kazi nae.

2. Jua kucheza na soko maana kama viazi vikijaa sokoni na bei pia hua chini ila vikiadimika utaoga faida.

3. Jazilizia mtaji angalau ufike 3M unaeza pata watu mkachanga mzigo mnapakia ndani ya gari moja.

NB: kumbuka ni mali kuoza hii usipocheza vzr mtaji unateketea wotee.
 
Back
Top Bottom