Biashara ya viazi soko la mabibo Dar es salaam

Sela Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,972
Reaction score
8,856
Mambo vipi wanajamvi! MTU wenu Leo Niko hapa kuulizia kuhusu biashara ya viazi kutoka huko vitokapo ( iringa,mbeya) mpaka kuingia sokoni Mabibo Dar es salaam. Kwa kuanza.
1_bei ya gunia moja shambani.
2-gharama za usafirishaji.
3-je nahitajika kuwa na leseni?
4-mbinu za ujanja ujanja sokoni
5-bei ya gunia sokoni.
Mwisho kabisa Nina TSH 1.2 milioni nataka kuanza biashara hii , either nikiwa Kama dalali au mfanyabiashara mpokezi kutoka kwa madalali na kuuza hapahapa sokoni!
Hili nimelileta ili kusaidiwa coz hapa ndani uwanjani hakifeli kitu.
Nawasilisha.
MTU wenu Sela son
 
Ukienda kufata iwe uyole sijui njombe.
Wasikubamize kwenye viazi kuna vingine cherema haviivi na havina soko.
Mbegu bora ni tigo halafu Obama na cp.

Nakushauri kafate mwenyewe shamba.
Ulete uuze na dalali sokoni(hapa hakuna cash cash tegemea hela baada ya siku 1,2 au 3)
Kwa hiyo hela nunua tu viazi na gharama zake kama magunia ushuru kamba upakiaji na ushushaji dar kuhusu gari tafuta za watu wengine wakupakilie mtalipana kwa gunia maana wewe mwenyewe huwezi kukodi gari yako kwa hela hiyo.
Bei ya soko kwa sasa ni 58,000 mpaka 65,000.
Bei ya shambani siijui.
Ukiwa serious zaidi kuna namba ya mkulima wa viazi ninayo nitakupa akusaidie kujua kuhusu huko shamba.
 
Kumbe akitokea dalali mwenye mtaji akanunua kwa cash anapata wauzaji wengi. Sijui kama changamoto atapata nyingi mpaka kumzuia asipate faida.
 
Hivi nani alikuambia dalali ana mtaji?
Wale madalali wa sokoni wanakujaga hawana sh mia mfukoni.
Hakuna dalali mwenye mtaji sokoni.
Wao wana maneno na dago tu kama mtaji wao na ukizubaa lazima akulize.
Kuhusu faida ipo hamna hamna hawezi kosa 3,000 mpaka 8,000 kwa gunia.
 
Je naweza kuchukua gunia ngapi kuleta jijini baada ya Makati yote ikiwemo usafiri? Mil 1.2
 
Sijakuelewa.
Kuitwa wewe kapuku na niliyoandika vinahusiana vipi? Huyo niliyekuitia ni master wa hiyo biashara ujue.
Ha ha, nimemaanisha aje huyo fundi atuelekeze Mimi na wanangu wengine tutoboe kimaisha mkuu,, tusiitwe makapuku tena
 
Hivi nani alikuambia dalali ana mtaji?
Wale madalali wa sokoni wanakujaga hawana sh mia mfukoni.
Hakuna dalali mwenye mtaji sokoni.
Wao wana maneno na dago tu kama mtaji wao na ukizubaa lazima akulize.
Kuhusu faida ipo hamna hamna hawezi kosa 3,000 mpaka 8,000 kwa gunia.
Ndo maana Niko hapa kuendelea kupata elimu,, kwa komenti yako ndipo kwa Mara ya kwanza nagundua madalali hawana hela
 
Nani alikuambia hawana hela?
Nimesema wanakujaga sh mia mfukoni hawana.
Wanategemea viazi vyako viwaletee hela h
Na mara nyingi wao ndo wanafaidika kuliko wewe mwenye mzigo au mkulima.
Dalali hawezi kuingia risk ya kutoa pesa yake akasafiri kwenda shamba na kuleta mzigo.
Atakusubiri sokoni umpelekee mzigo apige kazi.
Kirahisi kabisa.
 
Sawasawa br.
 
Kwa hiyo hela tafta masoko ya pembeni mfano tandika, tegeta, mbagala nk

Then unaenda kujumua viazi mabibo wewe unauza kwenye hayo masoko

Ukifikisha 3m ndipo uanze kujiingiza kupeleka viazi mabibo ukivichukua mikoani
 
Hivi nani alikuambia dalali ana mtaji?
Wale madalali wa sokoni wanakujaga hawana sh mia mfukoni.
Hakuna dalali mwenye mtaji sokoni.
Wao wana maneno na dago tu kama mtaji wao na ukizubaa lazima akulize.
Kuhusu faida ipo hamna hamna hawezi kosa 3,000 mpaka 8,000 kwa gunia.
Akitokea mtu smart hii fursa inawezekana. Akinunua kwa cash ananunua kwa bei punguzo maana wakulima hawatotaka risk ya kumwachia dalali wa kulipa baadae. Anachofanya huyu mnunuzi smart ni kuwa na hifadhi. Anakuwa dalali na msambazaji, ni kama retailer au market maker. Sema huo mtaji wake ni mrefu.
 
Je naweza kuchukua gunia ngapi kuleta jijini baada ya Makati yote ikiwemo usafiri? Mil 1.2
Mkuu mi mjingamjinga tu wala sijui chochote kwenye masoko. Mwenyewe nasoma tu hapa. Labda jaribu kutafuta nyuzi kama huu kisha saka watu waliotoa mchango, tag hapa au wafate wakuelekeze. Epuka matapeli.
 
Nani alikuambia hawana hela?
Nimesema wanakujaga sh mia mfukoni hawana.
Wanategemea viazi vyako viwaletee hela h
Na mara nyingi wao ndo wanafaidika kuliko wewe mwenye mzigo au mkulima.
Dalali hawezi kuingia risk ya kutoa pesa yake akasafiri kwenda shamba na kuleta mzigo.
Atakusubiri sokoni umpelekee mzigo apige kazi.
Kirahisi kabisa.
Ila madalali Ni noma saana. I wish niwe dalali. Unapiga hela bila kuwa na Mia mfukoni? Amazing
 
Back
Top Bottom