Fanya utafiki siyo kutaka tu. Hili ndilo tatizo la watu wengi. Akiwa na mpango badala ya kuufanyia utafiti anataka wengine wamtafunie. Maelezo ya hapa jamii hayawezi kukidhi shida yako. Just reaserch and think big my son.
Father of All,uliyosema ni kweli kabisa,ila inawezekana hana idea na hii biashara,kwa kweli hii biashara inahitaji refferals au agents wa kukuletea wageni,na utakuwa unacheza na exchange rates,kwa mikoa ya huku kaskazini hasa Arusha hii ndio biashara ya wengi.
ningefurahi kama ungekuwa more specific kuhusu utalii wa ndani maana kuna cultural tourism-ambayo wanatembelea vijijini,alternative tourism-kama volunteering,wildlife tourism,safari's,heritage,geo-tourism,film tourism....ziko nyingi sana.ukiwa specific ni maeneo gani unafanyia unaweza ukashauriwa vyema zaidi.
NB:mtaji ni mkubwa,by one way or another utahitaji gari ya watalii,,kwa mfano...nyingi ni landcruiser hardtop,used inatembea kwa M.20 za kitanzania,ukate mlango wa nyuma,kuweka bullbars,na ku-customize inaweza ikala 3M tena....kwa zile wanazoita war-bus,used zinapatikana kwa M.40.......na kwa kukodi si chini ya USD 200 kwa siku
thanx 4r advs, ninayo magali 2 ambayo mara nyingi naya tumia kukodisha. Na kuna kipindi yana baki nyumbani kwa muda mrefu .
Huu ndiyo mwanzo wa reserch nategemea mawazo yenu nikikusanya na ya kwangu napata kitu kizima.
Nime andika short ili kupata mawazo sahihi ya kila mchangiaji kwani nikitafuna kabisa nita pewa hongera tu kwa wazo nililo kuwa nalo bila kuchangia
Mkuu wazo ni zuri na labda kwa kuliongezea nyama ni kwamba huu utamaduni wa wazawa kutembelea vivutio vya asili ni mgeni kabisa katika jamii yetu, cha muhimu wewe ni muanzilishi (pioneer) kwa mantiki hii hakuna njia yakudumu zaidi yakujitangaza kwa njia ya kurasa mtandazo au njia yoyote ile nakufanya mtandao wakibiashara na watu wa hoteli na malazi ya bei rahisi, kujikita katika soko la wateja wako unaotaka kuwahudumia, pia utafiti ni muhimu kwa watu wenye uzoefu katika biashara hii ya utalii. Pia litumie soko la Afrika mashariki kama watu wa ndani. Kila la kheri.
same idea in a different way, kwa sasa naitunza kwanza hadi uwezo wangu utakapojitosheleza but all my eyes are on tours rite now. kila la kheri mkubwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.