Interesting story, jee wewe haya umejifunza wapi mkuu? au babu yako member? na hapo kwenye "red" ya kwanza kama wana maendeleo kama haya basi kwanini wasituletee na sisi tuka-advance katika technologia?. "red" ya pili jee kuna malipo au ukiwa member unahudumiwa bure? Jee kuna temporary/short term membership huko kwa wenye kutaka kujiunga? Niliwahi kusoma/kusikia kua huko wanaruka kwa ungo au fisi, sasa wewe unasema kuna ndege....hebu fafanua zaidi tuelimike.
De Javu. Shetani au Lucifier alipoadhibiwa na Mwenyenzi Mungu na kutupwa duniani, Mungu hakumwondolea uwezo wake wa kutenda na kufikiri. Aliondoka na akili zake na uwezo wake kikamilifu. Kumbuka kuwa alikuwa ni mmoja wa wasaidizi wa karibu sana na Mwenyenzi Mungu. Tunaweza kusema kuwa kwenye baraza la mawaziri la Mbinguni Lucifier alikuwa mmoja wao, hivyo alijuwa mambo mengi sana ya uumbaji na utendaji kazi wa Mbinguni.
Kwa taarifa yako asilimia kubwa ya technologia inayotumika duniani sasa hivi inatokea kuzimu. Utajiuliza inakuwakuwaje?
Zamani huko kijijini kwetu ilikuwa ni nadra sana kusikia kijana amefariki dunia, na linapotokea tukio kama hilo wazee walikuwa wanakaa na kulitafakari sana. Mambo yamebadilika sana sana sasa hivi, wewe mwenyewe ni shahidi, vijana wanapuputika kama majani. Je tatizo ni nini hasa? Je ni kwa sababu ya maendeleo, au ni kwa sababu ya magonjwa yasiyo na tiba, kila siku tunapoteza vijana wazuri wasomi.
Mwanzo nilieleza uwepo wa malango ya kuzimu, na hapa Tanzania yapo malango makuu saba ya kuzimu. Wapo wachawi wa nchi wanaongia huko na kutoka, unaweza kufikiri malango haya yapo chini sana ya ardhi kiasi kwamba ni lazima utafute kamba ya kushukia chini, lakini siyo. Utakuta malango haya karibu yote isipokuwa lango la Tabora na Njombe ndiyo yako nchi kavu. Mengine yako ziwani au baharini. Wachawi wa nchi wanapotaka kuingia ndani, kuna dua zao wanasoma na lango linajitokeza juu ya bahari au ziwa na lango hufunguka. Malango yote unashuka ngazi tatu peke yake, na mara unakuwa kwenye nchi nyingine tofauti kabisa, kuzimu ni kuzuri hakuna maelezo.
Utendaji kazi wa kuzimu ni kama wa huku duniani, ni sawasawa na unapoingia nchi nyingine ni lazima ujaze taarifa zako mpakani au uwanja wa ndege, utakuta wasichana wazuri ajabu wakikukaribisha na kujaza taarifa zako kwenye vitabu vya wageni, na baadaye unapelekwa kwa wahusika. Kuzimu ni miji mikubwa ajabu yapo magari, zipo nyumba, vipo viwanda na kila kitu kipo.
Kuzimu hawana shule nzuri, hivyo tegemeo lao ni vijana wanaohitimu katika vyuo mbalimbali huku duniani, ndio huchukuliwa kuzimu kuendeleza viwanda na shughuli mbalimbali za maendeleo, ndiyo maana zamani vijana walikuwa ni nadra sana kufariki hovyo kwa sababu hawakuwa na soko kuzimu kwa kuwa hawakuwa na elimu bora. Sasa hivi utasikia kijana msomi bingwa wa kutegemewa alilala hakuamka, aliumwa kichwa kesho yake kafa, gari yake ilipata ajali akafa. Ndiyo maana utakuta vijana wezi, wavuta bangi, mateja hawafi, hakuna kazi wanayoweza kuifanya kuzimu, hivyo huishi maisha yao ya hovyo hadi siku zao zifike hapa hapa duniani ndipo wanakufa.
Kuna aina mpya kabisa ya chombo cha usafiri usiotumia mafuta kinakuja, technologia hiyo italetwa duniani na nadhani kuna uwezekano mkubwa chombo hicho kikaanza kutengenezwa nchini Japan.
Ndege zipo, zinaitwa ndege za kichawi zipo, na mabasi ya abiria ya kuzimu yapo mbona mengi tu yapo barabarani, mengi yanaenda Tanga, Mombasa na Zambia. Magari ya kuzimu yapo mengi sana barabarani, hivi karibuni wapo wakulima walikuwa wanaleta viazi sokoni kutokea kigamboni, mara likafika gari aina ya toyota pickup double cabin, walilisimamisha na likasimama dreva akawaambia anaishia kigamboni, kwa sababu walikuwa wamechelewa sana wakakubali, wakapakia magunia yao nyuma na wao wakaingia wakakaa viti vya nyuma, lakini walishangaa walipofika feri walikuta feri ndiyo linaondoka, hivyo gari lao lilienda moja kwa moja ndani ya bahari, lakini walishangaa sana kwani hawakuyaona maji na wakajikuta katika nchi ya ajabu, kwa kudra za Mwenyenzi Mungu wajikuta wametupwa ufukweni Kunduchi.
Ndugu usikubali kabisa kuingia kwenye mambo ya uchawi, shetani ni mwongo kupindukia, atakupa utajiri wa kishindo lakini wa muda mfupi utakaoteketeza familia yako na wewe mwenyewe, ridhika na hali yako ya kusaga lami ukitafuta riziki lakini upate kuishi maisha marefu na familia yako ibaki salama.