Nahitaji hasa hiyo ndege
Kwa sababu nisizojua, kanisa moja mjini kwetu limefungwa, na mali zake zote zinauzwa. Pamoja na vitu vingine, kanisa hilo lilikuwa linamiliki broadcasting station ya kisasa yenye 330kW Digital UHF TV (high definition 1080i 16:9) na FM Radio 100kW Class C. Bei yake inaelekea ni nzuri tu, kwani nadhani wenyewe wanataka kuachana navyo tu; kiongozi wa kanisa hilo ameshauza ndege yake ndogo Piper Seminole PA-44 kwa $250,000 ambayo ni chini ya nusu ya bei yake.
Kama uko interested na vifaa hivyo wasiliana na mimi nikuunganishe na kanisa hilo.
Nyongeza: Mitambo hii inauzwa bila Antenna.
Ndege imeshauzwa; Vitu vingine vya maana vuilivyobaki zaidi ya jengo la kanisa na jengo broadcatsing station ni hiyo mitambo ya matanganzano niliyotaja hapo juu. Mimi binafsi nilitaka printing equipment zao za kutolea magazeti na vitabu lakini nikakuta zimeshauzwa.Nahitaji hasa hiyo ndege
Hzo mitambo za Tv bei gan?
Hawapangi bei; unatakiwa kutoa ofa yako, halafu wakiikubali basi unachukua, wasipoikubali watakuambia upande kidogo. Tafuta bei ya kuanzia- kama 35%-45% ya thamani halisi hivi, halafu niarifu nikuunganishe na pastor huyo
Basi hata ilo jengo tu nikipata itakuwa poa nihifadhie korosho maana msimu ndo umeanza ghal a za mtwara jpm(jupiter,pluto na mars) kageuza vitalu vya kuoteshea koroshoNdege imeshauzwa; Vitu vingine vya maana vuilivyobaki zaidi ya jengo la kanisa na jengo broadcatsing station ni hiyo mitambo ya matanganzano niliyotaja hapo juu. Mimi binafsi nilitaka printing equipment zao za kutolea magazeti na vitabu lakini nikakuta zimeshauzwa.
Samahani, kanisa lenyewe liko Marekani, kwa hiyo ukichukua jengo hilo kama boharia lako la korosho nadhani halitakusaida sana. Vitu vya muhimu ni vile vinavyohamishika kama nilivyotaja hapo juuBasi hata ilo jengo tu nikipata itakuwa poa nihifadhie korosho maana msimu ndo umeanza ghal a za mtwara jpm(jupiter,pluto na mars) kageuza vitalu vya kuoteshea korosho
mm nataka remote ya tv
Kanisa liko marekani tena? Usije ukakuta ni wanigeria wamekuweka kwenye mstari huko kwenye mitandao wakupige! Nakumbuka zile msg kuwa baba yangu kaniachia urithi wa £5m naomba account ili nitume pesa tuje tufanye Biashara, hahahaaaaSamahani, kanisa lenyewe liko Marekani, kwa hiyo ukichukua jengo hilo kama boharia lako la korosho nadhani halitakusaida sana. Vitu vya muhimu ni vile vinavyohamishika kama nilivyotaja hapo juu
Ni kanisa mzee wangu; mimi ni mtu mzima sana, siwezi kuleta jambo la uwongo hapa. Marekani kuna makanisa makubwa sana kama hujui, tena viongozi wa makanisa hayo ni matajiri sana. Utitiri wa makanisa uliotokea Tanzania miaka ya hivi karibuni ni kutokana na marekani; hata huyo Mchungaji rwakatare alisomea mambo hayo Marekani, akina Gwajima na Kakobe nao huwa wanakuja marekani mara kwa mara kutembelea na kujifunza kwenye makanisa hayo. Kanisa hili lililofungwa nadhani walikuwa na matatizo ya ama kukiuka sheria za kodi au lilikuwa na deni kubwa la benki au limekosa wafuasi sana kuweza kujiendesha; mimi siyo mfuasi wa kanisa hilo.Kanisa liko marekani tena? Usije ukakuta ni wanigeria wamekuweka kwenye mstari huko kwenye mitandao wakupige! Nakumbuka zile msg kuwa baba yangu kaniachia urithi wa £5m naomba account ili nitume pesa tuje tufanye Biashara, hahahaaaa