Biashara ya salon za kiume na kike

Leo naanza mchakato wa kutafuta chumba...
nitaleta update

Itakuwa vizuri pia akitokea mtu akatuwekea na bajet ya kufungua saloon ya kawaida inacost shilingi ngapi ni kwa kusaidia wengine wenye ndoto hizo.
 
kabla ya yote unavyo vifaa vya saloni au mpaka uvinunue?
na je eneo unalotaka kufungua biashara yako umelichunguza kwa makini
ukaona linafaa au wahitaji ushauri?

Kuhusu eneo ni vyema ukajua ni wapi waweza biashara yako inaweza kutoka
na kupata wateja na vilevile tambua ni mnyoaji gani anayefanya kazi kwa moyo
na anavutia wateja kwa lugha yake yenye ucheshi ukifahamu hayo ndipo anza kufungua hiyo biashara
Heshima kwenu.

Naomba kama kuna mtu ana uzoefu na saloon za kunyoa anipe uzoefu, tena zile za 1000 kichwa maana kwa hesabu zangu nikilipa chumba 40,000/50,000 na nikiongea na kinyozi anipe 10,000 kila siku na nikaiboresha si nitapata?
au mnanishauri vip?
 
Mahitajio ya awali kwa saluni ya kawaida-
1.chumba elfu 50
2.vioo laki 1.5
3.mashine mbili laki 2
4.Viti vya kunyolea 2 laki 2
5.Makochi laki 3
6.TV+Radio laki 3
7.Vitambaa,vitaulo,sprit,poda,mafuta,picha za mitindo,sabuni. vyote kwa elfu 50.
Jumla ni tsh 1,250,000/-
Aina hii ya salun kama ukipata eneo zuri kibiashara inaweza kukulipa.
 
Mahitajio ya awali kwa saluni ya kawaida-
1.chumba elfu 50
2.vioo laki 1.5
3.mashine mbili laki 2
4.Viti vya kunyolea 2 laki 2
5.Makochi laki 3
6.TV+Radio laki 3
7.Vitambaa,vitaulo,sprit,poda,mafuta,picha za mitindo,sabuni. vyote kwa elfu 50.
Jumla ni tsh 1,250,000/-
Aina hii ya salun kama ukipata eneo zuri kibiashara inaweza kukulipa.

Dah....!! Hii Budget mbona kama iko chini sana? ni kwa mkoa gani?
 
Dah....!! Hii Budget mbona kama iko chini sana? ni kwa mkoa gani?

mi naona kama ameandika bei ya juu maana mashine nataka kununua za 60,000@.
alafu TV,DEC,Kochi vyote ninavyo,na mashine moja tiyari ninayo.
 
Salon inalipa ila usimamie mwenyewe na location iwe ya ukweli ila kama ni mtu mwingine mtagawana faida tena atakuzidi labda umdhibiti kwa kusoma unit za umeme.

Lakini bado una appliances nyingi kama radio tv heater.
 
mi naona kama ameandika bei ya juu maana mashine nataka kununua za 60,000@.
alafu TV,DEC,Kochi vyote ninavyo,na mashine moja tiyari ninayo.
Mkuu mashine ya kunyolea ikiwa inauzwa chini ya laki kuwa makini kuikagua kama original ama na mara utajuta hyo mashine ni feki na kama ni feki baada mwezi 1ama 2 huanza kusumbua..

Kumbuka saloon ya kiume hakuna vitu muhim kama KINYOZI BORA NA MASHINE BORA..

Pia kutokana na bei ya room uliyoitaja elfu 40-50 inaonyesha ni room ya kawaida pia ni mtaan ambapo wateja Huwa ni cku Za w/end, kwa kuanzia j3 -ijumaa kupata elfu 10 pia kazi kodogo...

Ila idea nzur fanyia kazi..
 
Hivi wapi wana-train vijana wa kunyoa. Maana nataka nitafute vijawa wazuri kitabia niwatrain, then niwafungulie saloon wajitegemee.
 
Habari za asubuhi wakuu! Nataka kuwa mjasiriamali kwa kufungua biashara ya salon ya kisasa ya kiume, kwa mtu yeyote mwenye uelewa anijuze juu ya aina vifaa vinavyohitajika na bei ya kila kifaa. Pia ikiwezekana naomba kujua makadirio ya mtaji wa biashara hii.
 
Habari wana JF, nahitaji kuanzisha biashara ya saluni ya kunyoa nywele ila sijui nianze na mtaji wa kiasi gani? tafadhali kwa yeyote mwenye ideal karibu
 
Habari. Nataka kufanya biashara ya saloon ya kunyoa nywele wanaume pamoja na scrub. Naomba mnisaidie kujua gharama za vifaa vizuri vya saluni na upatikanaji wake. Mimi naishi mbeya na biashara itakuwa huko. Je mshahara wa kinyozi na mtu wa scrub kwa kuanzia huwa ni shilingi ngapi. Ushauri wenu utanisaidia mimi kutafuta mtaji sahihi wa kuanzia hii biashara .
 
mkuu kuna nyuzi nyingi humu zitakusaidia
ila nazani suala la mshahara ni maelewano tu ,kutokana na hadhi ya saloon!
Una mtaj kias gan mkuu?
 
Back
Top Bottom