Biashara ya 'Online shop'

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,483
40,498
Habari wananzengo!!!

Leo nakuja na hili wazo la biashara la 'online shop'

Kumekuwa na changamoto nyingi, hasa za kupata fremu ya duka maeneo mbali mbali. Na ikipatikana, bei inakuwa juu.

Kutokana na hiyo changamoto, unaweza kufanya kwa 'online shop'

Mahitaji

  • Lazima uwe na bidhaa ya kuuza (mzigo) i.e nguo, viatu, simu, mikoba n.k
  • Uwe na fremu (ofisi), iwe umeijenga nyumbani kwako, umepanga n.k
  • Fremu/ofisi, itengenezwe vizuri ionekane ni ofisi/ fremu ya duka
  • Panga bidhaa zako vizuri kwa umaridadi mkubwa, kwenye fremu /ofisi yako.
  • Uwe na laptop au simu nzuri ya kurekodi vitu vyako vyote vya dukani na kuvirusha mtandaoni; ni vizuri picha ya duka lote pamoja na bidhaa ziwe zinaonekana.
  • Rusha kwenye ma-'group' mbali mbali ya kimtandao, pamoja na bei ya bidhaa husika.
  • Anza kupokea oda, na wapelekee wateja.
 
Kufanikiwa katika online shop unahitaji vitu vitatu vikubwa
1. Bidhaa yenye demand katika jamii.
2.Bei poa ili watu wanunue kwa wingi
3.Network nzuri ya kilogistiki ya kudeliver na kureturn material, ili uweze kupeleka order siku ile ile au siku inayofuata(fast delivery).

Hii point ya tatu ndio muhimu zaidi ili kupata ufanisi mzuri, lakini uzuri wake unaweza kufanya ubia na kampuni nyengine ya transport kufanya hiyo kazi ya delivery.

Njia nyengine ni kufanya online platform
ambayo itawakutanisha wauzaji na wanunuzi kwa ajili ya kuwasiliana na kuuziana bidhaa, kazi yako itakuwa ni kumanage hiyo platform.
Muuzaji na mnunuzi wanawasiliana na mnunuzi kupitia chat iliyomo kwenye hiyo platform.
Vile vile unaweza kutumia online platform ambazo ziko tayari zinaruhusu mtu yeyote kuuza au kupost bidhaa kwa ajili ya kuuza online.
 
Habari wananzengo!!!

Leo nakuja na hili wazo la biashara la 'online shop'

Kumekuwa na changamoto nyingi, hasa za kupata fremu ya duka maeneo mbali mbali. Na ikipatikana, bei inakuwa juu.

Kutokana na hiyo changamoto, unaweza kufanya kwa 'online shop'

Mahitaji

  • Lazima uwe na bidhaa ya kuuza (mzigo) i.e nguo, viatu, simu, mikoba n.k
  • Uwe na fremu (ofisi), iwe umeijenga nyumbani kwako, umepanga n.k
  • Fremu/ofisi, itengenezwe vizuri ionekane ni ofisi/ fremu ya duka
  • Panga bidhaa zako vizuri kwa umaridadi mkubwa, kwenye fremu /ofisi yako.
  • Uwe na laptop au simu nzuri ya kurekodi vitu vyako vyote vya dukani na kuvirusha mtandaoni; ni vizuri picha ya duka lote pamoja na bidhaa ziwe zinaonekana.
  • Rusha kwenye ma-'group' mbali mbali ya kimtandao, pamoja na bei ya bidhaa husika.
  • Anza kupokea oda, na wapelekee wateja.
Changamoto no sababu ya kumfanya mtu aache kununua kwa mmachinga anatmyetembea,au wa barabarani aamue kukupigia Simu wewe umpelekee, changamoto ni Bei,Bei ya dukani/kwa mmachinga na yako ya kufayia delivery zitakuwa sawa? Magroup yako yako mangapi? Kwa siku yatafikia watu wamgapi? Watu wengi wamepoteza Imani ya BIASHARA za mtandao kwa sababu ya utapeli,wengi wamefanyiwa utapeli,kupelekewa vitu vibovu au ambavyo sivyo walivyoagiza,au kutapeliwabkabisa
 
Back
Top Bottom