Biashara ya omba omba inavyoshamiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya omba omba inavyoshamiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Oct 22, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  BIASHARA YA OMBAOMBA INAVYOSHAMIRI

  Ukiwa ndani ya daladala la kutoka mwenge kwenda posta au kariakoo kuna jambo Fulani unaweza kuona unapofika kituo cha makumbusho na Victoria nalo ni vijana waliokuwa pembeni hapo wakiomba hela toka kwa makondakta wa daladala .

  Hawa ni vijana wenye afya njema kabisa wameshiba wamevaa kinathifu lakini hutaka shilingi 200 au 300 toka kwa makonda wa hizo daladala na makonda huwa wanawapa hizo pesa muda mwingi inaonyesha kwamba wanaogopa kitu Fulani kama wasipotoa pesa kwa vijana hao .

  Wale wanaopita njia ya morogoro haswa eneo la fire kama unaenda mjini na magomeni wakati wa kurudi watakuwa wameona wakina mama wengi na wadada wa kike maeneo hayo ya vituo wakiomba pesa toka kwa wapita kwa miguu hata waendesha magari .

  Wengine wanafikia hatua hata ya kutuma watoto wao waoshe vioo vya magari ili wapate pesa kisha wanaenda kuwapa wale wakina mama na vibabu vilivyokaa pembeni mwa barabara vikiomba omba , inaonyesha biashara hii sasa hivi ina watu wake ambao wanafaidika kwa kiasi kikubwa ndio maana hakuna anayejali sana .
  Ukifika mtaa wa jamhuri katika eneo moja maarufu la azam wanapouza juice na ice cream kuna mzee mmoja pale ambaye miaka yote huwa anaomba omba , yeye ujanja wake ni kuficha mguu mmoja ili aonekane hana mguu ilihali mguu anao tena polisi wakifika eneo lile huwa anaweza kukimbia .

  Mzee huyu huwa anahama muda wa mchana anaenda eneo jingine kwenye mgahawa wa J J makutano ya morogoro road na samora ave , kutegemea na wateja wengi wako wapi ambao huenda kula ndani ya mgahawa huo .
  Maeneo ya posta ya zamani ndio utakutana na aina zingine za omba omba ambao huwa na vitoto vichanga wau watoto wadogo sana zaidi ya 2 hujifanya wamezalishwa halafu wanaume wamewakimbia kwahiyo wanaomba msaada wa kuweza kuwalea watoto wale kwahiyo siku zote wako wanaomba misaada hiyo haieleweki kwanini serikali za maeneo husika hazina mipango ya muda mrefu kwa ajili ya watu hawa .

  Hawa wakina mama huwa wanakodisha watoto hao kwa ajili ya biashara hizi nimewahi kuhisi hata haya mambo ya kuibiwa watoto ndani ya mahospitali inawezekana wakina mama hawa wanahusika kwa njia moja au nyingine

  Kama wewe unapenda kuchelewa kutoka mjini kuanzia saa 4 hivi au 5 usiku , ukipita maeneo ya magomeni mapipa angalia sana gari yako mara nyingi hao watoto wadogo wanaweza kuja kugonga kioo chako cha gari na kuvunja ukishituka wanafungua gari na kukuingilia ndani kisha utajua kitakachoendelea .

  Ukifika maeneo ya maenzese ndio balaa tupu , huwa wanatabia ya kurusha mawe au mchanga mbele ya kioo cha gari kama linatembea ili usimame waweze kukudhuru .
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du.. hii ni mambo ya kutisha sana!
  Mamlaka za miji kwa kushirikiana na vyombo vya dola wana uwezo wa kuondoa kama si kupunguza shida hii! Tatizo ni kwamba labda hakuna vogogo waliowahi kupata madhara ya mojakwa moja kuhusiana na adha ulizozieleza hapo juu!
   
Loading...