Biashara ya mpesa na maxmalipo zaingia utatani.

mwalidebe

JF-Expert Member
Mar 27, 2016
425
250
Baadhi ya mawakala wa mpesa na maxmalipo wamesitisha kutoa huduma zao kutokana na hasara kubwa ambayo wameipata.

Hali hii imejitokeza toka juzi ambapo mteja akitoa hela haiyonyeshi salio kwa wakala kama limeongezeka au la. Pia wakala akiweka hela kwa mteja haiyonyeshi kuwa hela imebaki kiasi gani.

Wakala mmoja amethibitisha kuwepo kwa tatizo hili nikimnukuu amesema
"salio langu lilikuwa laki mbili amekuja mteja nimuwekee elfu kumi baada ya kuweka hela ikaja sms inasema umefanikiwa kuweka elfu kumi na salio lililobaki ni sifuri sielewi pesa zangu zimekwenda wapi"

Kwa upande wa maximalipo ukiweka hela kwenye mashine kupitia mpesa ukifika mahali unaweka till yako wakati wa kuthibitishwa hutokea till nyingine.

Mwandishi wa habari hizi amejitahidi kuongea na vodacom hakufanikiwaa kuwapata.
 
Back
Top Bottom