Naomba msaada kuhusu biashara ya kuuza na Kubadilisha gesi

Naomba wajuzi mnipe mnipe mwongozo wake ukoje. Nataka kufungua hiyo biashara ila sikupata muda wa kumalizia utafiti wake kwa namna ya kujiunga kwa waingizaji wakuu na mie niwe msambazaji wao. Kuna madogo nataka wajikwamue na mie niingize za mboga, sasa nahitaji wazoefu mnipe mawazo yenu, madogo sio wa kuwamini sana maana bongo kama muijuavyo vishawishi sasa nikijua vingine toka kwa wadau naweza nikajiongeza mwenyewe.
Asanteni na poleni kwa uandishi wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utafiti wako uliishia wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbuzi ukimchunguza sana hutamla......

hakuna biashara inayolipa haraka labda uuze madawa tu. Mitungi hawawezi kukuibia hao madogo zaidi watakukimbia maana watakuwa hawaoni pa kukuibia. Labda akuambie mtungi umepotea, nimedondosha pesa nilizouza mtungi
 
kwanza uzuri wa hii biashara bidhaa zako zote zinahesabika vizuri pasipo na shaka, changamoto ni mzunguko wake inahitaji utafiti wa kutosha kuweza kupata eneo sahihi,au lenye afadhali yaan mzunguko wa iyo mitungi uwepo, pia ubunifu wa hali ya juu sana, mfano unaweza kufanya transportation free around 1.5km au chini ya apo au zaidi ya apo kulingana na usafiri ambao unao na kijana/vijana, unaweza wanunulia baskeli ya kawaida au ya kucharge ili wawe wanawapelekea wateja wanaacha na businss card hii mbinu ingesaidia kwa kiasi fulani, pamoja na mbinu nyingi za kunasa wateja,,,,,,,, mara nyingi maduka ya gas unawekamo na m-pesa, tigo pesa na related busnss kama izo.
 
Sawa nimekuelewa , shida yangu kubwa ni process za uwakala mkuu.

Sawa kabisa , delivery unaweza fanya mpaka 15 km bado faida ipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa nimekuelewa , shida yangu kubwa ni process za uwakala mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
wafuate mawakala wakuu ofisini ukawaulize watakupa utaratibu. Nadhani unatakiwa uwe na mtaji kiasi alafu wao wanakuja kukuletea mzigo unaotaka malipo unalipa kadri unavyouza taratibu. Nenda kila kampuni ya gesi unahitaji kuiuza mawakala wao watakupa utaratibu mzuri tu na rafiki kwa biashara yako. Huhitaji kuwa na mtaji mkubwa bali uaminifu wako
 
Asante sana kwa ushauri, mimi sipo hapo kwenye hilo zoezi ila nilitaka kupata maelezo toka kwa wadau ili vijana watakapo nipa mrejesho nilinganishe nione. Si unajuwa vijana wanaweza kukuletea na maelezo ya nyongeza ahaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4hrs hamna reply hata moja! ingekua mambo ya mapenzi na kutongoza kungekua na replies nyingi sana. anyways, kuna uzi nimeona mzuri nimekopi hii...

Anza hivi
Mtaji ni million 15
Nunua kirikou
Budget weka mil 7 utapata nzur tu
Nenda kwa super dealer wa gas nunua
Mitungi ya gesi
Midogo 100
Mikubwa 40
Midogo tupu 23000 ukijaza 15800 jumla 38800 × 100=3,880,000
Mikubwa tupu 42000 ukijaza 38000 jumla 80000×40=2,400,000
Jumla mtaji gas n 6,280,000 ukijumlisha na kirikou 13,200,00
Kodi ya stock ya gas itakapokaa 50,000×6=300,000
Vibali +Kumodify body ya kirikou ges zikae ktk uzio wa machuma+mengineyo weka 500,000
Jumla mil 14,000,000 cash
Hio million moja baki nayo km balance kwa dharura
*unasupply kwenye maduka ya reja reja ya gesi
*wewe ndio dereva wewe ndio salesman
*mtungi mdogo unauzwa 17000 mkunbwa 41000 kwa wiki hukosi kusambaza 600units -400 units kwa daresalaam maana miduka n mengi sana
*kapge kazi mchanganuo huo hapo uje na ushuhuda hapa*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mtaji. Mhh lkn ahsante kwa mchanganuo, umenifungua akili
Huo mtaji umechangamka na kwenye mchanganuo Kuna makosa kidogo ukiufuatisha Kama ulivyo mbeleni unakwama.
Kwa mfano kwenye bei ya kirikuu sio milioni 7 bali ni zaidi ya milioni 9.
Na kwenye kodi ya frem 50000tsh ni nje ya mji halaf mtaani ila Kama ni maeneo ya centre kodi inaanzia 150000tsh kwa mwezi.
Na Kuna vitu vingine vimekosekana Kama kodi ya tra n.k.
 
Habari wakuu, baada ya kuhangaika na cv sana maofisini...... Sasa naomba nijuzwe nataka kufanya hii biashara nipo Mbeya ambaye amewai kufanya hii biashara Msaada kuhusu mtaji na faida kwa kila mtungi na mchanganuo wake kwa undani faida na hasara.. Nawasilisha
 
Nitafute nikupe fursa ya tamu km u jasiri utapiga pesa mpk ulete ushuhuda hapa.

Pitia pm.

Back
Top Bottom