Kuna tajiri mmoja siku nilikuta anampiga makofi mfanyakazi wake wa kike....
Jamaa alikua na cashpoint sijui Hawa matapeli wanatumia njia gani wakaja kubadilisha alivyo save jina la bosi wake, dada akaanza kuombwa miamala kutoka Kwa bosi Kuna namba akawa anamuelekeza atume pesa huko Kuna magari yake yamekwama kuchukua mzigo....Kila baada ya muda anaambiwa atume pesa kwenye namba flani, miamala mizito mizito tu..... Mpaka float akaishiwa akawa anataka kwenda kujaza float ndo akakutana na mtu wanafahamiana na bosi wake, yule mtu anamuuliza mbona huku tena ofisini umemuacha nani? Ndo dada anamwambia bosi Leo msumbufu Kila saa anaomba pesa mpaka nimeishiwa float, jamaa ndo akamuambia subiri kwanza akampigia bosi wake, bosi kufika aisee anaangalia miamala alipiga ukunga nusu amuue mtoto wa watu.....
Boss anadai alishampiga marufuku kumtumia pesa hata awe na shida gani ni heri akachukue sehemu nyingine, lakini ndo hivo tena jamaa wakapita na zaidi ya 10M+