Biashara ya mazao

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari wana JF

Mimi ni kijana mtafutaji kama walivyo wengine wengi katika pita pita zangu nikaona fursa

Fursa yenyewe ni kuuza nafaka ambazo zimeshaongezwa thamani tayari

Ili kufanikisha hilo nikaona ni bora nianze na mahindi pamoja na mpunga kwanza wakati nasubiri mtaji kukua

Sehemu ya kupata malighafi kuprocess nafaka na masoko vyote nimepitia na nishaweka sawa tayari

TATIZO: changamoto ambayo nimeona nije kuwashirikisha ni katika swala zima la kufungasha product yangu kwani nikiyekubaliana nae kuprocess iyo malighafi hana viroba wala mashine ya kushonea viroba hivyo

OMBI: Nilikuwa naomba kwa yeyote mwenye kufahamu sehemu wanapouza mashine za kushonea viroba ivyo na pia wapi naweza pata viroba kwa ajili ya kufungashia bidhaa yangu na kama nitapata mtu wa kuwa anaviprint vizuri ili viwe na muonekano mzuri

SHUKRAN: Napenda kuwashukuru nyote kama mtanisaidia na mawasiliano yao itanifaa zaidi ahsanteni
 
Me nipo Songea Nembo wanatengeneza kwa laki na Nusu halafu unaanza kuprint unauziwa vifungashio kuanzia sh 300, 400, 500 kulingana na ukubwa wa kifungashio mashine za kushonea zinauzwa 250,000 na kuendelea kulingana na aina ya mashine.
 
Toa namba za hawa wahusika tafadhali
 
Back
Top Bottom